Featured Kitaifa

DKT.BITEKO AIPONGEZA EWURA KWA USIMAMIZI MZURI WA USHIRIKI WA KAMPUNI ZA NDANI KATIKA MRADI WA EACOP

Written by mzalendoeditor

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mh. Dkt.Doto Mashaka Biteko ameipongeza EWURA kwa kusimamia vizuri ushiriki wa Kampuni za ndani katika mradi wa EACOP kwa mujibu wa sheria na mikataba ya mradi.

Amesema hatua hiyo imefanikisha kubaini baadhi ya watanzania wasiokuwa waaminifu ambao hujisajili kwa kutumia Kampuni za nje ili kutambulika kama kampuni ya ndani na kupatiwa kazi ndani ya mradi.

Dkt. Biteko amepongeza hatua hiyo leo tarehe 25.4.2024 Bungeni wakati akihitimisha hoja ya Bajeti ya Wizara yake kwa Mwaka wa Fedha 2024/25.

About the author

mzalendoeditor