Photos

DKT NCHEMBA ATETA NA MKURUGENZI MTENDAJI BENKI YA DUNIA KUNDI LA AFRIKA

Written by mzalendo
Ujumbe wa Tanzania (kushoto) ukiongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), ukiwa katika kikao na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia Kundi la Kwanza la nchi za Kanda ya Afrika (Africa Group 1 Constituency), Dkt. Floribert Ngaruko, Makao Makuu ya Benki hiyo jijini Washington D.C, nchini Marekani, wakati wa mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), ambapo wamejadiliana masuala mbalimbali yanayohusu ushirikiano kati ya Benki ya Dunia na Tanzania.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (kushoto), na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia Kundi la Kwanza la nchi za Kanda ya Afrika (Africa Group 1 Constituency), Dkt. Floribert Ngaruko, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa kikao chao kilichofanyika Makao Makuu ya Benki hiyo, jijini Washington D.C, nchini Marekani, wakati wa mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), ambapo wamejadiliana masuala mbalimbali yanayohusu ushirikiano kati ya Benki ya Dunia na Tanzania.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia Kundi la Kwanza la nchi za Kanda ya Afrika (Africa Group 1 Constituency), Dkt. Floribert Ngaruko (Katikati), akizungumza wakati wa kikao na ujumbe wa Tanzania ulioongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), kilichofanyika Makao Makuu ya Benki hiyo jijini Washington D.C, nchini Marekani, wakati wa mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), ambapo wamejadiliana masuala mbalimbali yanayohusu ushirikiano kati ya Benki ya Dunia na Tanzania. Wengine katika picha ni Mkurugenzi Mtendaji Mbadala wa Benki ya Dunia, anayewakilisha Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika (Africa Group 1 Constituency (AfG1), Dkt. Zarau Kibwe (kushoto), Mshauri wa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia, anayewakilisha Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika (Africa Group 1 Constituency (AfG1), Bw. Venuste Ndikumwenayo (kulia).
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (katikati), Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia Kundi la Kwanza la nchi za Kanda ya Afrika (Africa Group 1 Constituency), Dkt. Floribert Ngaruko (wa tatu kulia), Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (wa tatu kushoto), Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Fedha na Mipango-Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil (wa pili kulia), Mkurugenzi Mtendaji Mbadala wa Benki ya Dunia, anayewakilisha Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika (Africa Group 1 Constituency (AfG1), Dkt. Zarau Kibwe (wa kwanza kulia), Mshauri wa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia, anayewakilisha Kundi la Kwanza la Nchi za Afrika (Africa Group 1 Constituency (AfG1), Bw. Venuste Ndikumwenayo ( wa pili kushoto) na Afisa Idara ya Fedha za Nje, Bw. Charles Longo (wa kwanza kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kikao chao kilichofanyika Makao Makuu ya Benki ya Dunia, jijini Washington D.C, nchini Marekani, wakati wa mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), ambapo wamejadiliana masuala mbalimbali yanayohusu ushirikiano kati ya Benki ya Dunia na Tanzania.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Washington D.C)
Na Joseph Mahumi, WF, Washington
 
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia Kundi la Kwanza la nchi za Kanda ya Afrika (Africa Group 1 Constituency), Dkt. Floribert Ngaruko, wakati wa mikutano ya Majira ya Kipupwe (Spring Meetings) ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) jijini Washington D.C, Nchini Marekani, ambapo wamejadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Benki hiyo na Tanzania.

About the author

mzalendo