Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis akitoa salamu wakati wa Maonesho ya Biashara Miaka 60 ya Muungano katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo Aprili 19, 2024 ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Cyprian Luhemeja akitoa neno la ukaribisho wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Biashara Miaka 60 ya Muungano katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo Aprili 19, 2024 ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.
Washiriki mbalimbali wakifuatilia ufunguzi wa Maonesho ya Biashara Miaka 60 ya Muungano katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo Aprili 19, 2024 ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.
……..
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis amewahimza Watanzania kutafakari na kutathmini masuala muhimu yaliyokusudiwa na waasisi wa Muungano.
Amesema kupitia waasisi hao Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume ambao walitia saini Hati ya Makubaliano ya Muungano tunapaswa kuimarisha umoja, amani na utulivu wa taifa waliotuachi.
Mhe. Khamis amesema hayo wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Biashara Miaka 60 ya Muungano katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam leo Aprili 19, 202, ambapo mgeni rasmi alikuwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar wa Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla.
Amesema maonesho haya ni mfululizo wa shughuli mbalimbali zinazoratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais katika kutoa elimu ya Muungano kwa makundi mbalimbali wakiwemo wananchi, wabunge, viongozi wa Serikali, wanafunzi pamoja na makundi mengine.
Mhe. Khamis ambaye alimwakilisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira Mhe. Dkt. Selemani Jafo amesema ambaye alimwakilisha Wazutamaduni huu ni kielelezo tosha cha mshikamano na uhusiano mzuri baina ya pande mbili ili kuendelea kudumisha Muungano huu adhimu.
“Kama mnavyofahamu Ofisi ya Makamu wa Rais ndio yenye dhamana ya Masuala ya Muungano, Ofisi hii ilianzishwa miaka 60 iliyopita, hivyo sambamba na maadhimisho ya Miaka 60 ya Muungano ya Tanganyika na Zanzibar nayo Ofisi ya Makamu wa Rais itatimiza miaka 60 mwezi Aprili mwaka huu tangu kuanzishwa kwake mwaka 1964,” amesema.
Pia, Mhe. Khamis amesema kuwa mara baada ya Tanganyika na Zanzibar zilipoungana tuliainisha mambo 22, hivyo, kupitia maonesho haya wananchi watapata fursa ya kufahamu huduma zinazotolewa na Taasisi za Muungano.
Ametaja mengine kuwa ni mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 60 ya Muungano kwa wananchi wa pande zote mbili za Muungano na pia kupata fursa ya kutoa maoni na ushauri utakaowezwsha kuimarisha na kudumisha muungano wetu. Kwa kipekee na cha kufurahisha utafahamu chimbuko, msingi na maendeleo ya Muungano wetu uliodumu kwa miaka 60 sasa.
Ameongeza kuwa uchumi umeimarika kutokana na mazingira na mahusiano mazuri ya kibiashara kati ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar.
Kutokana na ushirikiano huo amesema taasisi za Muungano zilizopo Tanzania Bara zimefungua Ofisi Zanzibar ambapo hadi sasa Taasisi 33 zimefungua Ofisi Zanzibar kati ya Taasisi 39 za Muungano.