Featured Kitaifa

TARURA INAFANYA KAZI KUBWA YA KUGUSA MAISHA YA WATU- MHE. KATIMBA

Written by mzalendo

Na Mwandishi Wetu, Dodoma.

Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Zainab Katimba amewapongeza Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kwa kazi kubwa wanayofanya ya kumsaidia Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuunganisha barabara za wilaya nchini.

Mhe. Katimba ameyasema hayo leo Aprili 9,2024 , alipokutana na kufanya kikao na Menejimenti ya TARURA kwenye ukumbi wa Wakala uliopo mji wa Serikali-Mtumba jijini Dodoma.

Amesema TARURA inafanya kazi kubwa ya kugusa maisha ya watu na ustawi wa jamii kila siku kwani barabara wanazozijenga zinaenda kutoa Huduma za kijamii pamoja na zile za kiuchumi.

“Watanzania wana matarajio nasi,hivyo mjipange na kuwe na jitihada za kuleta suluhishi hususan msimu wa mvua ”. 

Hata hivyo amesema waendelee kuwa wabunifu,washirikiane na kutatua changamoto pale panapotokea dharura.

Naye, Mtendaji Mkuu wa TARURA Mhandisi Victor Seff amesema wamefanya kazi kubwa ya kurudisha Mawasiliano maeneo yaliyokumbwa na Elnino hususan maeneo ya kutolea Huduma za kijamii.

About the author

mzalendo