Featured Kitaifa

MAKAMU WA RAIS ATOA SADAKA YA FUTARI KWA WANANCHI WA WILAYA YA MAFIA

Written by mzalendo

Wananchi mbalimbali wa Wilaya ya Mafia mkoani Pwani wakijumuika katika futari iliyoandaliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango aliyoitoa kwaajili ya wakazi wa Wilaya hiyo hususani watu wa makundi maalum wakiwemo walemavu, wazee na watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

……

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango ametoa sadaka ya futari kwa Wakazi wa Wilaya ya Mafia mkoani pwani hususani watu wa makundi maalum wakiwemo walemavu, wazee na watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

Akitoa shukrani kwa niaba ya wananchi wa Mafia mara baada ya futari hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Mafia Bi. Aziza Mangosongo amemshukuru Makamu wa Rais kwa sadaka aliyotoa kwa watu wa Mafia na kuahidi kwamba wananchi wa Wilaya hiyo wataendelea kuwaombea heri na baraka viongozi wote. 

Mkuu wa Wilaya amewasihi wananchi wa eneo hilo kuendelea kujitoa kwaajili ya wengine wakati huu wa mfungo Mtukufu wa Ramadhani na hata baada ya mfungo. Amewaasa wananchi wa Wilaya hiyo kutenda mema kama ambavyo mwezi Mtukufu wa Ramadhani unavyofunza pamoja na kuendelea kuchangia katika masuala muhimu kwaajili ya Mwenyezi Mungu ikiwemo katika nyumba za ibada.

Pamoja na sadaka ya futari pia watoto wanaoishi katika mazingira magumu wamekabidhiwa vitendea kazi vya kusomea ikiwemo madaftari na kalamu kwaajili ya kuwasaidia mashuleni.

Wananchi mbalimbali wa Wilaya ya Mafia mkoani Pwani wakijumuika katika futari iliyoandaliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango aliyoitoa kwaajili ya wakazi wa Wilaya hiyo hususani watu wa makundi maalum wakiwemo walemavu, wazee na watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

About the author

mzalendo