Featured Kitaifa

DK. NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA

Written by mzalendo

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk. Emmanuel John Nchimbi, amemtembelea kumjulia hali mmoja wa Makatibu Wakuu Wastaafu wa CCM, Mzee Yusuf Makamba, Jumatatu, Aprili 1, 2024, nyumbani kwake jijini Dar Es Salaam.

Akimpongeza kwa kuteuliwa kushika nafasi hiyo na kumtakia heri kwenye majukumu hayo mapya, Mzee Makamba amemzawadia Balozi Dk. Nchimbi shati moja la sare ya Chama Cha Mapinduzi, ikiwa ni ishara ya kifaa cha kazi, ambapo Katibu Mkuu huyo wa CCM, alipokea pongezi na kumshukuru kwa zawadi hiyo.

About the author

mzalendo