Featured Kitaifa

BALOZI KASIKE ATETA NA WAZIRI WA KILIMO WA ESWATINI

Written by mzalendo

Mhe. Balozi Phaustine Kasike, akutana na Waziri wa Kilimo wa Ufalme wa Eswatini, Mhe. Mandla Tshawuka, tarehe 28 Machi, 2024.

Mkutano huo ulifanyika katika Ofisi za Wizara ya Kilimo ya Ufalme wa Eswatini Jijini Mbabane ambapo Viongozi hao wawili walisisitiza haja ya kusainiwa Hati ya Makubaliano (MoU) itakayorasimisha mahusiano hayo na pia kueleza maeneo na namna ambavyo nchi hizi zitashirikiana katika Sekta ya Kilimo.

Kwa upande mwingine, Serikali ya Eswatini iliwasilisha ombi la kununua mifugo kutoka Tanzania, ambapo Mhe. Balozi Kasike aliahidi kulifikisha kwenye Mamlaka husika kwa hatua za maamuzi.

Imetolewa na Ubalozi wa Tanzania – Maputo
28 Machi, 2024

About the author

mzalendo