Featured Kitaifa

JELA MAISHA KWA KOSA LA KULAWITI

Written by mzalendo

Mahakama ya Wilaya Singida ememuhukumu kwenda jela maisha kijana Mohamed Jumanne ambaye pia anajulikana kwa jina la Salanda, (22) Mkulima na Mkazi wa VETA, Kata ya Utemini, Manispaa ya Singida kwa kosa la kulawiti.

Mshitakiwa Mohamedi alitenda kosa hilo Machi 27, 2023 kwa kumlawiti mtoto mwenye umri wa miaka 7 katika maeneo ya VETA ambapo Jeshi la Polisi limefanya upelelezi wa tukio hilo na kumkamata mtuhumiwa huyo kisha kufikishwa mahakamani Mei 10, 2023.

Aidha, Mahakama hiyo imetoa hukumu hiyo baada ya pande zote mbili za Jamhuri na upande wa Mshitakiwa kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.

Hukumu hiyo imetolewa Machi 27, 2024 mbele ya Mh. Fadhili Ennock Luvinga Hakimu Mfawidhi Mahakama ya Wilaya Singida.

About the author

mzalendo