Featured Kitaifa

RAIS DK. MWINYI APOKEA SALAMU ZA POLE KUTOKA AMREF IKULU ZANZIBAR

Written by mzalendo

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Ujumbe wa Amref ukiongozwa na Waziri wa Afya Tanzania Mhe.Ummy Mwalimu (kushoto kwa Rais) na (kulia kwa Rais) CEO wa Amref Dr.Githinji Gitahi, walipofika Ikulu Jijini Zanzibar kwa kutowa Salamu za Pole na mazungumzo, kufuatilia kifo cha Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Pili Hayati Alhajj Ali Hassan Mwinyi, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Zanzibar.21-3-2024.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa  zawadi maalum ya Salamu za Pole kutoka Amref na Mkurugenzi Mkuu wa Amref Tanzania Dr.Florence Temu, baada ya kumaliza mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar 21-3-2024.(Picha na Ikulu)   

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na Waziri wa Afya Tanzania Mhe.Ummy Mwalimu na CEO wa Amref Dr. Hithinji Gitahi, baada ya kumaliza mazungumzo yao na kutowa salamu za pole kufuatia kifo cha Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Pili Hayati Alhajj Ali Hassan Mwinyi, mazungumzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar 21-3-2024.(Picha na Ikulu)  

About the author

mzalendo