Featured Kitaifa

KICKSTART YAENDESHA KONGAMANO LA WADAU WA KILIMO CHA UMWAGILIAJI SHINYANGA

Written by mzalendo

 

 Afisa Kilimo kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga bi. Ancila Karani akifanya majaribio namna Pampu ya Money Maker Max  inavyofanya kazi

 

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

 
Shirika la KickStart International limeendesha Kongamano la wadau wa Kilimo cha Umwagiliaji Mkoa wa Shinyanga ili kuinua umwagiliaji kwa wakulima wadogo Kusini mwa Jangwa la Sahara Afrika ukiwemo mkoa huo huku likitambulisha Pampu za Umwagiliaji za Money Maker.
 
Kongamano hilo limefanyika leo Ijumaa Machi 22,2024 Mjini Shinyanga likikutanisha wadau mbalimbali wa Kilimo ambapo Mgeni rasmi alikuwa Afisa Kilimo kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga bi. Ancila Karani kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo.
 
Akizungumza wakati wa Kongamano hilo, Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga bi. Ancila Karani amelipongeza na kulishukuru Shirika la KickStart International kwa kuwekeza kwenye Kilimo cha Umwagiliaji kwani ni noja ya vipaumbele vya serikali katika kufikia ajenda ya 10/30 ambayo inagusa pia kilimo cha umwagiliaji, huduma za ugavi, zana za kilimo na tafiti za masoko.
Afisa Kilimo kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga bi. Ancila Karani akizungumza kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo
 
“Tunawashukuru Kick Start International wamejikita kwenye hoja ya kipaumbele cha serikali cha umwagiliaji ambayo ni sehemu ya malengo ya serikali kufikia ajenda ya 10/30 ambapo tunataka kuhakikisha kilimo kinakua kwa asilimia 10 ifikapo mwaka 2030 na mkoa wa Shinyanga umeweka kipaumbele suala la Kilimo cha umwagiliaji”,amesema Karani.
 
“Serikali ina vipaumbele vingi na haiwezi kubeba kila eneo na ndiyo maana kuna wadau kama nyie na kila mmoja wenu amegusa eneo flani ili kusukuma gudurumu la maendeleo na hasa kwa kuwagusa wakulima. Wakulima wadogo ni muhimu sana kwa sababu zaidi ya asilimia 60 ya chakula kinatoka kwa wakulima wadogo”,ameongeza Karani.
 
Aidha ameliomba shirika la KickStart International kuhakikisha mashine hizo zinapatikana kwa urahisi kwa wakulima kwa kuzipeleka kwa wauza pembejeo.
 
Kwa upande wake, Meneja wa Shirika la KickStart International Tanzania bw. Mwaluko Mpangwa amesema lengo la kongamano la wadau wa kilimo cha umwagiliani ni kuwa na matokeo chanya kwa wakulima kwani dhima ya KickStart International ni kuwainua wakulima.
Meneja wa Shirika la KickStart International Tanzania bw. Mwaluko Mpangwa.
 
“Sisi tunafanya kazi kupitia ushirikiano na wadau wa kilimo na ndiyo maana katika Kongamano letu tumekutana na mashirika na wadau mbalimbali wa kilimo ili kuunganisha nguvu ili tunapoenda kule chini kwa wakulima tunapeleka matokeo chanya kwa wakulima ili kumsaidia mkulima kwa ujumla wake”,amesema Mpangwa.
 
Amesema kutokana na kwamba kumekuwa na ongezeko la kutokuwa na uhakika wa mvua na hata kubashiri kwake hivyo ili mkulima asiyumbe mara mvua zinapokosekana ndiyo maana KickStart International wamekuja na Pampu za Umwagiliaji za Money Maker.
 
“Siri ya kuongeza mavuno hadi mara 10 inaanzia kwa wewe kuwa na teknolojia sahihi ya umwagiliaji. Utaweza kuvuna mara nyingi katika mwaka, mazao yaliyozalishwa kwa kumwagiliwa vizuri hadi kukomaa kwake yanatoa mavuno makubwa na yenye ubora lakini pia mkulima anapata fursa ya kupata bei nzuri wakati majira ya kiangazi”,ameeleza Mpangwa.
Wadau wa Kilimo cha Umwagiliaji wakiwa ukumbini.
 
“Baada ya ajenda ya umwagiliaji tumeenda mbali zaidi, tumekuja na teknolojia ya umwagiliaji zinazosaidia wakulima,nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara Afrika ndiyo zimeathirika zaidi na mabadiliko ya tabia nchi kwa sababu tumekuwa tukitegemea zaidi mvua, lakini masuala ya lishe na usalama wa chakula, mazingira. Kwa hiyo tuna teknolojia rahisi ambazo tunawapatia wakulima ili waongeze uzalishaji. Kupitia teknolojia hizi rahisi tulizonazo mkulima atainuka kiuchumi kwa gharama nafuu”,ameongeza Mpangwa.
 
Akielezea kuhusu Pampu za Money Maker, Meneja wa Ubia na Mauzo wa KickStart International bw. Ernest Jerome amesema pampu hizo hazitumii umeme au mafuta, ni rahisi kuziandaa na kuzitumia, ni nyepesi zinabebeka kirahisi,zinafungashwa pamoja na spea zake, spea zinapatikana kwa urahisi katika maduka ya pembejeo na hazihitaji matengenezo ya mara kwa mara.
Meneja wa Ubia na Mauzo wa KickStart International bw. Ernest Jerome akielezea kuhusu Pampu ya Money Maker Max.
 
“Tuna Pampu ya Money Maker Max inayoendeshwa kwa kukanyaga kwa miguu ambayo ina uwezo kwa kumwagilia hadi ekari 2 kwa siku hii kwa bei ya jumla inauzwa shilingi 450,000/= kama unachukua nyingi kuna punguzo. Lakini pia tuna Pampu ya Money Maker Starter, hii ni toleo letu jipya la pampu zetu yenye gharama ya chini zaidi kiasi cha shilingi 250,000/= kwa bei ya rejareja. Ni rahisi kuiandaa na kuitumia iwapo shambani na ni msaada mkubwa kwa wakulima kuvuka kutoka kumwagilia kwa kutumia ndoo”,ameongeza Jerome.
 
 
Nao wadau walioshiriki Kongamano hilo akiwemo Meneja wa World Vision Tanzania Kanda ya Ziwa bi. Jaequeline Kaihura wameishukuru KickStart International kwa kuwakutanisha pamoja wadau wa kilimo na kwamba ushirikiano huo utasaidia kumuinua mkulima hivyo kuboresha kipato kwa ajili ustawi wa jamii ikiwa ni kuunga mkono jitihada za World Vision katika kukuza ustawi wa mama na mtoto.
 
Miongoni mwa wadau walioshiriki kongamano hilo ni MEDA Tabora na Kahama, CARITAS Shinyanga, REDESO,Compassion, Mratibu wa Mradi wa NOURISH,REACT na Growth- Enrich, Vision Fund Tanzania, TCRS, Agrovets, Ofisa wa Tume ya Umwagiliaji Shinyanga, Maafisa Kilimo wilaya ya Kishapu, Shinyanga, Kahama na Nzega, TIDO na MVIWATA.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mgeni Afisa Kilimo kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga bi. Ancila Karani akizungumza kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo wakati wa Kongamano la wadau wa Kilimo cha Umwagiliaji Mkoa wa Shinyanga lililoandaliwa naShirika la KickStart International leo Ijumaa Machi 22,2024 Mjini Shinyanga – Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mgeni Afisa Kilimo kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga bi. Ancila Karani akizungumza kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo wakati wa Kongamano la wadau wa Kilimo cha Umwagiliaji Mkoa wa Shinyanga lililoandaliwa na Shirika la KickStart International
Meneja wa Shirika la KickStart International Tanzania bw. Mwaluko Mpangwa akizungumza wakati wa Kongamano la wadau wa Kilimo cha Umwagiliaji Mkoa wa Shinyanga lililoandaliwa na Shirika la KickStart International
Meneja wa Shirika la KickStart International Tanzania bw. Mwaluko Mpangwa akizungumza wakati wa Kongamano la wadau wa Kilimo cha Umwagiliaji Mkoa wa Shinyanga lililoandaliwa na Shirika la KickStart International
Mwakilishi wa Katibu Tawala Wilaya ya Shinyanga, Neema Mukandala akizungumza wakati wa Kongamano la wadau wa Kilimo cha Umwagiliaji Mkoa wa Shinyanga lililoandaliwa na Shirika la KickStart International
 Meneja wa Ubia na Mauzo wa KickStart International bw. Ernest Jerome akizungumza wakati wa Kongamano la wadau wa Kilimo cha Umwagiliaji Mkoa wa Shinyanga lililoandaliwa na Shirika la KickStart International
Meneja wa Ubia na Mauzo wa KickStart International Kanda ya Ziwa, Samwel Maganga akizungumza wakati wa Kongamano la wadau wa Kilimo cha Umwagiliaji Mkoa wa Shinyanga lililoandaliwa na Shirika la KickStart International
Meneja wa World Vision Tanzania Kanda ya Ziwa bi. Jaequeline Kaihura akizungumza wakati wa Kongamano la wadau wa Kilimo cha Umwagiliaji Mkoa wa Shinyanga lililoandaliwa na Shirika la KickStart International
Meneja wa Kanda ya Afrika Mashariki KickStart International, Pascal Maitha akitoa wasilisho kuhusu shughuli zinazofanywa na KickStart international wakati wa Kongamano la wadau wa Kilimo cha Umwagiliaji Mkoa wa Shinyanga lililoandaliwa na Shirika la KickStart International
Meneja wa Ubia na Mauzo wa KickStart International bw. Ernest Jerome akiwaelezea wadau wa kilimo cha umwagiliaji kuhusu Pampu ya Money Maker Max  inayoendeshwa kwa kukanyaga kwa miguu yenye uwezo kwa kumwagilia hadi ekari 2 kwa siku
Meneja wa Ubia na Mauzo wa KickStart International bw. Ernest Jerome akionesha kwa vitendo namna Pampu ya Money Maker Max  inavyofanya kazi
Onesho kwa vitendo namna Pampu ya Money Maker Max  inavyofanya kazi likiendelea
Mdau wa Kilimo cha Umwagiliaji, Mratibu wa Mradi wa NOURISH unaotekelezwa na Shirika la World Vision Tanzania, bi. Irene Abusheikh akifanya majaribio namna Pampu ya Money Maker Max  inavyofanya kazi
Meneja wa Ubia na Mauzo wa KickStart International bw. Ernest Jerome akiwaelezea wadau wa kilimo cha umwagiliaji kuhusu Pampu ya Money Maker Starter yenye gharama ya chini zaidi kiasi shilingi 250,000/= na ina uwezo mkubwa
Meneja wa Ubia na Mauzo wa KickStart International bw. Ernest Jerome akiwaelezea wadau wa kilimo cha umwagiliaji kuhusu Pampu ya Money Maker Starter
Kongamano la wadau wa Kilimo cha Umwagiliaji likiendelea
Kongamano la wadau wa Kilimo cha Umwagiliaji likiendelea
Kongamano la wadau wa Kilimo cha Umwagiliaji likiendelea
Kongamano la wadau wa Kilimo cha Umwagiliaji likiendelea
Kongamano la wadau wa Kilimo cha Umwagiliaji likiendelea
Wadau wa Kilimo cha Umwagiliaji wakipiga picha ya kumbukumbu
Wadau wa Kilimo cha Umwagiliaji wakipiga picha ya kumbukumbu
 
Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

About the author

mzalendo