Featured Kitaifa

JELA MAISHA KWA KULAWITI

Written by mzalendo

Na Mwandishi Wetu, Kagera.

Mahakama ya Wilaya ya Bukoba Mkoa wa Kagera imemuhukumu mshitakiwa Jonas George, mkulima,mkazi wa mtaa wa Kashai katika manispaa ya Bukoba kifungo cha maisha jela baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kumlawiti mtoto wa kiume (10) mwanafunzi wa darasa la tatu.

Mshitakiwa alitenda kosa hilo Novemba 04,2023 majira ya saa kumi na mbili asubuhi huko katika mtaa wa Kashai manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera baada ya kumrubuni madhula.

Akitoa hukumu hiyo March 13,2024 hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Bukoba mheshimiwa Kabuka amesema kuwa Mahakama imejiridhisha pasipo na shaka ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka na hatimaye kumtia hatiani mshitakiwa kwa kosa hilo.

Mshitakiwa huyo amehukumiwa kifungo hicho ili iwe fundisho kwa wahalifu wanao jihusisha na vitendo vya ukiukaji wa sheria,maadili na ukatili dhidi ya watoto.

About the author

mzalendo