Featured Kitaifa

ASILIMIA 40 YA WANAWAKE WANAFANYIWA UKATILI

Written by mzalendo

Na. Mwandishi Wetu, Dodoma .

Tafiti zilizofanywa nchini Tanzania zinaonesha kuwa asilimia 40 za wanawake waliopo kwenye umri wa miaka 15 Hadi 49 wamefanyiwa ukatili wa kijinsia ikiwemo kupigwa, kukatwa viungo na kuchomwa moto ambapo kati ya wanawake 100 , 40 wameumizwa na wenza wao .

Aidha chimbuko la ukatili huo ni ukosefu wa kutambua usawa kati ya wanawake na wanaume, ikiwa ni imani na mazoea kwamba ukatili wa kijinsia unakubalika ndani ya jamii

Tafiti hizo zimetolewa na Kaimu Kamishina Wizara ya Maendeleo ya Jamii ,Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Tullo Marijani Katika siku ya utepe mweupe ambapo uhadhimishwa kila Mwaka ifikapo March 15 .

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Uchechemuzi na Mawasiliano Save Children Victoria Marijani amesema kuwa Katika kuunga juhudi za Serikali
Wanashirikiana na serikali katika kuhakikisha watoto wanatambua haki zao za msingi pamoja na kutambua maeneo ya kwenda Kutoa Taarifa endapo watafanyiwa vitendo vya ukatili.

“LENGO ni kumfanya mtoto apate haki ya kuishi,haki ya kulindwa, haki ya kujifunza na kupata lishe iliyo bora ili Taifa liwe na rasilimali watu ambao Wenye nguvu na Tija”. Amesema Masanja

Naye Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya ushauri ya watoto na vijana save the children Tanzania Nancy Kasembo amesema kama Bodi ya ushauri anawakilisha vijana katika Kutoa maoni chanya na Masuala ya ukatili namna gani watoto na vijana kuwa vinara wa kupinga ukatili lakini pia wakatoa Elimu kwa vijana na watoto wakapaza sauti zao katika kuhakikisha wanatengeneza Taifa lililobora na imara.

Kauli mbiu ya Mwaka huu inasema kujenga kizazi kilicho salama kwa kukomesha ukatili wa kijinsia na watoto Tanzania Kwa kupitia vijana wa shule.

About the author

mzalendo