Kitaifa

OFISI YA WAZIRI MKUU ITAENDELEA KURATIBU PROGRAMU YA ASDP II ILI KUONGEZA TIJA” DKT. YONAZI

Written by mzalendo

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akizungumza kuhusu masuala ya ASDP II wakati wa kikao kuhusu Maendeleo ya zoezi la tathmini na uhuishaji wa Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II) kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi hiyo jijini Dodoma tarehe 13 Machi, 2024.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Bw. Anderson Mutatembwa akifuatilia wasilisho wakati wa kikao kuhusu Maendeleo ya zoezi la tathmini na uhuishaji wa Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II) kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi hiyo jijini Dodoma.

Mwakilishi wa AGRA nchini, Bw. Vianey Rweyendela akichangia jambo wakati wa kikao hicho.

Mratibu wa Kitaifa wa Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili(ASDP II) Dkt. Salim Nandonde akizungumza jambo wakati wa kikao kuhusu Maendeleo ya zoezi la tathmini na uhuishaji wa Programu hiyo katika ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dodoma tarehe 13 Machi, 2024 Jijini Dodoma.

Afisa Programu Mkuu kutoka Taasisi ya Axum Tanzania Bw. Malik Nkuba akiwasilisha wasilisho wakati wa kikao kikao kuhusu Maendeleo ya zoezi la tathmini na uhuishaji wa Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II) kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu jijini Dodoma tarehe 13 Machi, 2024 Jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi (katikati), Naibu wake Bw. Anderson Mutatembwa (kushoto kwake) wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kikao kuhusu Maendeleo ya zoezi la tathmini na uhuishaji wa Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II) katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi hiyo jijini Dodoma tarehe 13 Machi, 2024 Jijini Dodoma.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

NA. MWANDISHI WETU – DODOMA

KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi ameeleza kuwa, Ofisi yake itaendelea kuratibu Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II) ili kuendelea kuleta tija kwenye sekta hiyo.

Ameyasema hayo alipokutana na timu ya wataalamu kwa lengo la kujadili Maendeleo ya zoezi la tathmini na uhuishaji wa Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II) tarehe 13 Machi, 2024 katika ukumbi wa Ofisi hiyo Jijini Dodoma.

Kikao hicho kilijumuisha wataalam kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Idara ya Sera na Uratibu wa Shughuli za Serikali, Wasimamizi wa Programu ya ASDP II, Wataalam kutoka AGRA pamoja na Taasisi ya Axum Tanzania.

Dkt. Yonazi ameeleza kuwa adhima ya Serikali ni kuhakikisha Sekta ya Kilimo inaendelea kupewa kipaumbele ili kuinua uchumi wa Taifa na kujiletea maendeleo.

About the author

mzalendo