Kitaifa

TFS WASHIRIKI KONGAMANO LA WANAWAKE LA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

Written by mzalendo

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) ni moja ya Taasisi ambayo imeshiriki kwenye Kongamano la Wanawake la Nishati Safi ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.

Akizungumza na vyombo vya habari Mhifadhi Anna Lyauo katika banda lao amesema Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) ni mdau mkubwa katika kuhakikisha kwamba matumizi safi ya Nishati.

“Ile Nishati chafu ni ile inayotokana na matumizi ya kuni,kuni zenyewe ukizichoma zinatoa hewa ya kaboni ambayo inaenda kuchafua anga”amesema.

“Sisi tunahamasisha watu wasikate miti ili tuwe na hali ya hewa nzuri,hivyo watu watumie gesi ambayo ndiyo Nishati Safi kwa sababu yenyewe ukiitumia haina madhara katika anga”amesema.

Aidha amesema TFS wameendelea kuhamasisha watu wapande miti ni katika kuokoa hali ya anga ambayo tayari ishachafuka na kuongeza kuwa viongozi mbalimbali wa Serikali wanaungana katika kuhakikisha miti haikatwi.

Kuhusu kutoa elimu kwa jamii juu ya Utunzaji wa Mazingira amesema kuwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania TFS ina vipindi mbalimbali ambavyo ni vya kuhamasisha watu kutokutumia kuni,ikiwa ni pamoja na kutumia maonyesho mbalimbali, vipindi vya radio, vipindi vya TV ambavyo vinatangaza na kuhamasisha Umma watumie gesi badala ya kuni ili kuweza kuhifadhi zaidi Mazingira

“Lakini pamoja na hayo tuna gari ambalo lina sinema linatembea katika maeneo mbalimbali hususani katika zile sehemu ambazo hazina umeme na hazifikiki kwa urahisi lengo ni kuhamasisha watu wasikate miti”

About the author

mzalendo