Featured Kitaifa

SERA YA JINSIA NA MAENDELEO YA WANAWAKE NI MUHIMU KUKUZA USAWA WA KIJINSIA

Written by mzalendo
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima,akizungumza wakati wa  maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya wanawake Machi 08, 2024 yaliyofanyika Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa
…….
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amesema Sera ya Jinsia na maendeleo ya Wanawake ni ya muhimu katika kukuza usawa wa kijinsia hasa kutokana na kuweka kipaumbele kwa ushiriki wa wanaume katika jitihada za kujenga usawa wa Kijinsia. 
Hayo yamesemwa kwa niaba yake na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima katika maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya wanawake Machi 08, 2024 yaliyofanyika Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma.
Amebainisha kwamba anaamini Sera hiyo itaivusha Tanzania katika kipindi kingine kirefu katika utekelekezaji wake ili kuendana na Dira ya Taifa ya Maendeleo na Malengo ya Dunia kuhusu usawa wa kijinsia. 
“Natambua kuwa kazi ya mapitio ya sera haikuwa rahisi kwani ilihitaji ushiriki wa wadau na rasilimali fedha. Hivyo, nawashukuru wadau wote walioshirikiana na Serikali kukamilisha mapitio hayo ikiwemo wananchi waliotoa maoni, wadau wa maendeleo wa ndani na nje ya Nchi, Asasi za Kiraia, Taasisi Binafsi na Wataalam kutoka Wizara zote na Taasisi za Serikali. Vilevile natoa rai kwa wadau kuhakikisha wanatoa ushirikiano katika utekelezaji wa Sera hii.” Amesema Waziri Dkt. Gwajima.
Ametumia nafasi hiyo pia kuainisha baadhi ya jitihada zinazofanywa na Serikali katika kuwainua wanawake nchini katika nyanja mbalimbali hasa elimu, maji, nishati nafasi za uongozi na afya ambapo inaonesha hatua kubwa iliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza idadi ya wanawake wanaonufaika.  
Waziri Dkt. Gwajima amewasisitiza wanawake kujiunga vikundi vya maendeleo ili kutumia fursa za kiuchumi zinazotolewa na Serikali pamoja na wadau na kuwahimza kujitokeza kugombea nafasi mbalimnali za uongozi katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu.
Aidha, ametoa wito kwa wadau wote kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa Sera hiyo ili iwanufaishe Wananchi wote na kuwaasa wananchi kuungana kupinga vitendo vya  ukatili nchini.
Akieleza lengo la Sera hiyo mpya ya Jinsia na Maendeleo ya Wanawake, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jinsia Badru Abdulnuru amebainisha kuwa  ni kutokana na changamoto zilizokuwepo kwenye Sera ya mwaka 2000 kutokidhi hali halisi ya mahitaji ya sasa.
Naye Balozi Kaganda kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwasilisha maelezo ya wadau wa Kimataifa,  amesema wadau wanapongeza Serikali kwa uamuzi wa kuzindua Sera  mpya na kuona umuhimu wa ushirikishwaji wa wanawake katika masuala mbalimbali. Wanaahidi kiendelea kushirikiana kuhakikisha sera hiyo inawafikia walengwa wote.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Majukwaa ya uwezeshaji wanawake kiuchumi mkoa wa Dodoma Mary Nambaya amewasisitiza wanawake kujiunga na vikundi vya kijamii na kiuchumi na kuomba Serikali na wadau kuangalia changamoto ya masharti magumu ya mikopo na riba kubwa.
u inayosema “Wekeza kwa wanawake: Kuharakisha Maendeleo ya Taifa na ustawi wa Jamii”.

About the author

mzalendo