Featured Kitaifa

SIDO YATOA MAFUNZO KWA VIJANA UTENGENEZAJI WA VIHENGE MRADI WA TANIPAC KUDHIBITI SUMUKUVU

Written by mzalendoeditor
Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo na Usimamizi wa Mikoa SIDO, Stephen George Bondo akizungumza na kuonesha vihenge vilivyotengezwa na vijana walioshiriki mafunzo yaliyotolewa na SIDO kuhusu utengenezaji wa Vihenge kupitia mradi wa Kuzuia Sumukuvu wa TANIPAC ulio chini ya Wizara ya Kilimo ili kuimarisha usalama wa chakula kwa wananchi na afya ya jamii.
 
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) limetoa mafunzo kwa vijana 23 kuhusu utengenezaji wa Vihenge kupitia mradi wa Kuzuia Sumukuvu wa ‘Tanzania Initiative for Preventing Aflatoxin Contamination – TANIPAC)‘ ulio chini ya Wizara ya Kilimo ili kuimarisha usalama wa chakula kwa wananchi na afya ya jamii.

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo leo Jumamosi Machi 9,2024 katika ukumbi wa SIDO Shinyanga, Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo na Usimamizi wa Mikoa SIDO, Stephen George Bondo amesema mafunzo hayo yaliodumu kwa muda wa Wiki mbili, yamewapa vijana hao mbinu mbalimbali ya utengenezaji vihenge kwa vitendo, ujasiriamali, masoko, usimamizi wa fedha na urasimishaji biashara.
 
“Mradi wa PANIPAC unalenga kuwawezesha jamii kutumia njia sahihi na za kisasa za uhifadhi wa nafaka hususani mahindi kutokana na sumukuvu. Serikali imeingia gharama kuhakikisha kuwa vijana wanapatiwa ujuzi wa kutengeza vifaa vya kisasa na vinavyodumu kwa muda mrefu ili kutimiza adhima ya kupunguza sumukuvu”,amesema Bondo.
“Nendeni mkatumie kwa vitendo mafunzo haya ili kutimiza malengo yaliyokusudiwa ambayo pia yatawawezesha kuongeza kipato cha mtu mmoja mmoja, kaya na taifa kwa ujumla. Mkawe waalumu wa kufundisha vijana wenzenu ili kwa pamoja tuweze kupambana kwa vitendo kutokomeza sumukuvu. Haya ni mafunzo awamu ya kwanza tutaendelea kutoa mafunzo ya namna hii awamu zingine”,ameongeza Bondo.
 
Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa SIDO Mkoa wa Shinyanga bi. Misuka Makwaya amewasihi washiriki wa mafunzo hayo wakayatumie kwa vitendo ili kutimiza malengo ya serikali ya kutokomeza sumukuvu na wakawe mabalozi wa kukemea matumizi yasiyo sahihi ya utunzaji wa nafaka yanayopelekea sumukuvu.
 
Akisoma Risala ya wahitimu wa mafunzo hayo, Josephat Jonathan Makorogo amesema mafunzo hayo yalianza Februari 26,2024 hadi Machi 9,2024 yakiwa na washiriki 23 kutoka Mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Geita.
 
Makorogo amesema katika mafunzo hayo wamejifunza kuhusu ujasiriamali,masoko na huduma kwa wateja, usimamizi wa fedha, urasimishaji wa biashara na utengenezaji wa vihenge kwa vitendo.
 
“Elimu na mafunzo tuliyopata yatatusaidia kuboresha utendaji kazi na kuzalisha bidhaa za vihenge (Silos) na nyinginezo kwa tija ili kukidhi mahitaji ya soko la ndani na nje ya nchi. Tunaishukuru uongozi wa SIDO na Wizara ya Kilimo kwa kutoa fursa ya mafunzo haya ambayo yametujengea uwezo wa kujiamini na kuamsha ari ndani yetu ya kujiajiri na kuachana na kasumba ya kusubiri ajira”,amesema Makorogo.
 
Hata hivyo amesema licha ya kupata ari ya kujiajiri wanakabiliwa na changamoto ya mitaji kwa ajili ya kununua vitendea kazi vya kuanzisha shughuli mbalimbali kutokana na fani walizojifunza ili waweze kujiajiri na kuajiri wengine hivyo kuchangia uchumi wao na jamii na kutokomeza kabisa Sumukuvu nchini.
Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo na Usimamizi wa Mikoa SIDO, Stephen George Bondo akiangalia vihenge vilivyotengezwa na vijana walioshiriki mafunzo yaliyotolewa na SIDO kuhusu utengenezaji wa Vihenge kupitia mradi wa Kuzuia Sumukuvu wa TANIPAC ulio chini ya Wizara ya Kilimo
Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo na Usimamizi wa Mikoa SIDO, Stephen George Bondo akizungumza na vijana walioshiriki mafunzo yaliyotolewa na SIDO kuhusu utengenezaji wa Vihenge kupitia mradi wa Kuzuia Sumukuvu wa TANIPAC ulio chini ya Wizara ya Kilimo
Muonekano wa vihenge vilivyotengezwa na vijana walioshiriki mafunzo yaliyotolewa na SIDO kuhusu utengenezaji wa Vihenge kupitia mradi wa Kuzuia Sumukuvu wa TANIPAC ulio chini ya Wizara ya Kilimo
Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo na Usimamizi wa Mikoa SIDO, Stephen George Bondo akizungumza wakati akifunga mafunzo ya utengenezaji wa Vihenge kupitia mradi wa Kuzuia Sumukuvu wa TANIPAC ulio chini ya Wizara ya Kilimo.
Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo na Usimamizi wa Mikoa SIDO, Stephen George Bondo akizungumza wakati akifunga mafunzo ya utengenezaji wa Vihenge kupitia mradi wa Kuzuia Sumukuvu wa TANIPAC ulio chini ya Wizara ya Kilimo

 Kaimu Meneja wa SIDO Mkoa wa Shinyanga bi. Misuka Makwaya akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya utengenezaji wa Vihenge kupitia mradi wa Kuzuia Sumukuvu wa TANIPAC ulio chini ya Wizara ya Kilimo

Josephat Jonathan Makorogo akisoma risala ya wahitimu wakati wa kufunga mafunzo ya utengenezaji wa Vihenge kupitia mradi wa Kuzuia Sumukuvu wa TANIPAC ulio chini ya Wizara ya Kilimo
Washiriki wa mafunzo ya utengenezaji wa Vihenge kupitia mradi wa Kuzuia Sumukuvu wa TANIPAC ulio chini ya Wizara ya Kilimo

Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo na Usimamizi wa Mikoa SIDO, Stephen George Bondo (kulia) akimkabidhi cheti mmoja wa washiriki wa mafunzo ya utengenezaji wa Vihenge kupitia mradi wa Kuzuia Sumukuvu wa TANIPAC ulio chini ya Wizara ya Kilimo

Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo na Usimamizi wa Mikoa SIDO, Stephen George Bondo, viongozi wa SIDO Shinyanga wakipiga picha ya kumbukumbu na washiriki wa mafunzo ya utengenezaji wa Vihenge kupitia mradi wa Kuzuia Sumukuvu wa TANIPAC ulio chini ya Wizara ya Kilimo

Kaimu Mkurugenzi wa Mafunzo na Usimamizi wa Mikoa SIDO, Stephen George Bondo, viongozi wa SIDO Shinyanga. wakipiga picha ya kumbukumbu na washiriki wa mafunzo ya utengenezaji wa Vihenge kupitia mradi wa Kuzuia Sumukuvu wa TANIPAC ulio chini ya Wizara ya Kilimo
 
Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
 
About the author

mzalendoeditor