Kitaifa

CMA YAENDELEA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA MAHAKAMA KUU DIVISHENI YA KAZI

Written by mzalendo

Mkurugenzi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA), Usekelege Nahshon Mpulla, Kaimu mkurugenzi wa Usuluhishi, Rodney Matalis pamoja na Kaimu mkurugenzi wa Uamuzi, Valensi Wambali, leo Machi 07,2024 wamekutana na kufanya mazungumzo na Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Mheshimiwa Dkt.Yose Mlyambina, jijini Dar es salaam.

Mazungumzo haya yanalenga kuboresha mahusiano mazuri baina ya Tume ya Usuluhishi na Uamuzi CMA pamoja na mahakama kuu Divisheni ya Kazi katika utatuzi wa migogoro ya Kikazi Tanzania bara.

Tume imekua ikiendeleza mahusiano mazuri na taasisi mbalimbali Tanzania ikiwa na lengo la kuendelea kutoa huduma bora kwa jamii kwa kuendelea kuhudumia watanzania na wawekezaji kutoka nje ya Tanzania na wazawa.

About the author

mzalendo