Kitaifa

TAGCO WAKABIDHI MSAADA KWA AJILI YA  WAHANGA WA HANANG’

Written by mzalendo

Na Mwandishi Weyu.

Makamu Mwenyekiti Chama cha Maofisa Mawasiliano Serikali (TAGCO), Bi. Nteghenjwa Hosea, amekabidhi msaada wa mavazi kwa Katibu Tawala Mkoa wa Arusha Missaile Albano Musa, kwa ajili ya kuuwasilisha mkoani Manyara kwa Wahanga wa Maafa yaliyotokea mji mdogo wa Katesh wilaya ya Hanan’g,mwishoni mwa mwaka 2023.

Makamu Mwenyekiti Nteghenjwa, amekabidhi msaada huo, kwa niaba ya Wananchama TAGCO waliojitoa kwa ajili ya watanzania wenzao, waliokumbwa na maafa hayo Mkoani Manyara. 

Wanachama hayo wa TAGCO wametoa msaada huo, mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wao wa mwaka 2024, uliofanyika kwa siku tatu kwenye Kituo cha Mikutano ya Kimataifa Arisha (AICC) Jijini  Arusha. 

Katibu Tawala huyo, amewashukuru wananchama wote kwa kutambua thamani ya kutoa hasa kwa watu waliokumbwa na maafa, akisistiza kuwa hiyo ni sadaka ambayo Mwenyenzi Mungu ameibariki.

About the author

mzalendo