Featured Kitaifa

RAIS SAMIA ASHIRIKI KATIKA MAZISHI YA RAIS MSTAAFU MZEE MWINYI MANGAPWANI ZANZIBAR

Written by mzalendo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Viongozi wengine mbalimbali wakiomba Dua ya pamoja kabla ya mazishi ya  Rais Mstaafu wa awamu ya pili Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi yaliyofanyika Kijijini kwake Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja tarehe 02 Machi 2024

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi pamoja na Viongozi mbalimbali wakiswali  Swala ya Maiti mbele ya Jeneza lenye mwili wa Rais Mstaafu wa awamu ya pili Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi kabla ya kuzikwa Kijijini kwake Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja tarehe 02 Machi 2024.

Bibi Siti Mwinyi Mjane wa Rais Mstaafu wa awamu ya pili Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi na Familia yake wakiwa katika Simanzi na majonzi wakati Jeneza lenye mwili wa Hayati Mzee Mwinyi likitolewa mara baada ya kuswaliwa kuelekea kwenye Makaburi kwa ajili ya Mazishi yaliyofanyika Kijijini kwake Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja tarehe 02 Machi 2024.

Viongozi Wastaafu mbalimbali wakiwa katika kisomo na Dua kabla ya mazishi ya Rais Mstaafu wa awamu ya pili Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi yaliyofanyika Kijijini kwake Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja tarehe 02 Machi 2024.

About the author

mzalendo