Featured Kitaifa

DKT. BITEKO ASISITIZA UMUHIMU WA EREA SEKTA YA NISHATI

Written by mzalendo

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amekutana na kuzungumza na Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Udhibiti wa huduma za Nishati kwa nchi za Afrika Mashariki (EREA) Dkt. Geoffrey Mabea leo tarehe 26 Februari, 2024 jijini Dar es Salaam.

Kikao hicho kimejadili masuala mbalimbali ya nishati kwa nchi wanachama na umuhimu wa kujenga uwezo wa Wataalam katika Sekta ya Nishati ili kuongeza tija na huduma bora kwa wananchi.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Waziri wa Maji, Nishati na Madini wa Zanzibar Mhe. Shaib Kaduara na Wataalam kutoka EREA. 

About the author

mzalendo