Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kulia), na Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dkt. Patricia Laverley, wakisaini hati za Mikataba miwili yenye thamani ya takribani dola za Marekani milioni 158.1 (sawa na shilingi za Tanzania, bilioni 398.7) kwa ajili ya ujenzi wa Mradi wa Kimataifa wa Reli ya Kisasa (SGR) utakaoziunganisha nchi ya Tanzania, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), pamoja na kuiongezea mtaji Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini (TADB), hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Hazina Ndogo, jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (Mb), Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje, Bw. Rished Bade, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Bw. Masanja Kadogosa, Mwakilishi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania, Bw. Emmanuely Lyimo na viongozi wengine waandamizi wa Serikali.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kulia), na Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dkt. Patricia Laverley, wakionesha hati za Mikataba miwili yenye thamani ya takribani dola za Marekani milioni 158.1 (sawa na shilingi za Tanzania, bilioni 398.7) kwa ajili ya ujenzi wa Mradi wa Kimataifa wa Reli ya Kisasa (SGR) utakaoziunganisha nchi ya Tanzania, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), pamoja na kuiongezea mtaji Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini (TADB), hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Hazina Ndogo, jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (Mb), Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje, Bw. Rished Bade, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Bw. Masanja Kadogosa, Mwakilishi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania, Bw. Emmanuely Lyimo na viongozi wengine waandamizi wa Serikali.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza katika hafla ya utiaji saini Mikataba miwili yenye thamani ya takribani dola za Marekani milioni 158.1 (sawa na shilingi za Tanzania, bilioni 398.7) kwa ajili ya ujenzi wa Mradi wa Kimataifa wa Reli ya Kisasa (SGR) utakaoziunganisha nchi ya Tanzania, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), pamoja na kuiongezea mtaji Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini (TADB), katika ukumbi wa Mikutano wa Hazina Ndogo, jijini Dar es Salaam, na kushuhudiwa na Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (Mb), Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje, Bw. Rished Bade, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Bw. Masanja Kadogosa, Mwakilishi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania, Bw. Emmanuely Lyimo na viongozi wengine waandamizi wa Serikali.
Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Makame Mbarawa (Mb), akizungumza katika hafla ya utiaji saini Mikataba miwili yenye thamani ya takribani dola za Marekani milioni 158.1 (sawa na shilingi za Tanzania, bilioni 398.7) kwa ajili ya ujenzi wa Mradi wa Kimataifa wa Reli ya Kisasa (SGR) utakaoziunganisha nchi ya Tanzania, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), pamoja na kuiongezea mtaji Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini (TADB), iliyotiwa saini na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) nchini, Dkt. Patricia Laverley, katika ukumbi wa Mikutano wa Hazina Ndogo, jijini Dar es Salaam.
Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) nchini, Dkt. Patricia Laverley, akizungumza katika hafla ya utiaji saini Mikataba miwili yenye thamani ya takribani dola za Marekani milioni 158.1 (sawa na shilingi za Tanzania, bilioni 398.7) kwa ajili ya ujenzi wa Mradi wa Kimataifa wa Reli ya Kisasa (SGR) utakaoziunganisha nchi ya Tanzania, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), pamoja na kuiongezea mtaji Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini (TADB), katika ukumbi wa Mikutano wa Hazina Ndogo, jijini Dar es Salaam, na kushuhudiwa na Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (Mb), Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje, Bw. Rished Bade, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Bw. Masanja Kadogosa, Mwakilishi wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania, Bw. Emmanuely Lyimo na viongozi wengine waandamizi wa Serikali.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (katikati), Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Makame Mbarawa (Mb) (wa pili kulia), Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (wa kwanza kulia), na Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dkt. Patricia Laverley (wa pili kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na timu kutoka AfDB, baada ya hafla ya utiaji saini Mikataba miwili yenye thamani ya takribani dola za Marekani milioni 158.1 (sawa na shilingi za Tanzania, bilioni 398.7) kwa ajili ya ujenzi wa Mradi wa Kimataifa wa Reli ya Kisasa (SGR) utakaoziunganisha nchi ya Tanzania, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), pamoja na kuiongezea mtaji Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini (TADB), iliyotiwa saini na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) kwa niaba ya Serikali ya Tanzania na Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dkt. Patricia Laverley, katika ukumbi wa Mikutano wa Hazina Ndogo, jijini Dar es Salaam.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Dar es Salaam)
Na. Farida Ramadhani na Joseph Mahumi, WF, Dar es Salaam
Tanzania na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) zimesaini mikataba miwili yenye thamani ya zaidi dola za Marekani milioni 158.1 (shilingi za Tanzania bilioni 398.7) kwa ajili ya ujenzi wa Mradi wa Kimataifa wa Reli ya Kisasa (SGR) utakaoziunganisha nchi za Tanzania, Burundi na Jamhuri ya Kidemikrasia ya Kongo pamoja na kuiongezea mtaji Benki ya Maendeleo ya Kilimo nchini (TADB).
Hafla ya utiaji saini wa mikataba hiyo imefanyika jijini Dar es Salam kati ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba na Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) nchini, Dkt. Patricia Laverley.
Akizungumza baada ya kusaini mikataba hiyo, Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba alisema kati ya fedha hizo, dola milioni 91.76 (shilingi bilioni 231.3) ni kwa ajili ujenzi wa reli ya kisasa kutoka kipande cha sita (Lot 6) chenye urefu wa kilomita 411 kutoka Tabora hadi Kigoma na kipande cha saba (Lot 7) chenye urefu wa kilomita 156 kutoka Uvinza hadi Malagarasi.
Alisema mradi huo utaunganishwa na bandari ya Dar es Salaam kupitia mradi unaondelea wa ujenzi wa reli ya SGR kutoka Dar es Salaam – Morogoro – Makutupora – Isaka – Tabora (Lot 1, 2, 3 na 4), kwa lengo la kuiunganisha Tanzania na nchi ya Burundi kupitia reli ya kisasa kutoka Malagarasi hadi Musongati Burundi yenye urefu wa kilomita 84 na baadae iungane na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kutokea Malagarasi.
“Mradi huu wa reli ya kisasa, unalenga kuimarisha uchukuzi kwa njia ya reli na kufanya biashara ya madini na kilimo pamoja na kuimarisha mahusiano ya kikanda na wenzetu wa Burundi na Kongo”, alibainisha Dkt. Nchemba.
Alisema fedha hizo zilizosainiwa ni sehemu ya kiasi cha dola za Marekani milioni 502.69 zinazohitajika kukamilisha mradi huo ambapo AfDB imeahidi kudhamini nchi katika masoko ya mitaji ili kuweza kupata fedha zilizobakia na kutekeleza adhma yake ya kuimarisha miundombinu ya uchukuzi nchini.
Aidha, Dkt. Nchemba alisema kuwa mkataba wa pili uliosainiwa unathamani ya dola za Marekani milioni 66 (shilingi bilioni 166.4) kwa ajili ya kuongeza mtaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) ili kuendeleza Sekta ya Kilimo nchini.
Alisema fedha hizo zinalenga kuwezesha wananchi wa Tanzania kupata mitaji kwa ajili ya shughuli za kilimo ili kuongeza uzalishaji, kuimarisha usalama wa chakula, kukuza biashara ya bidhaa zinazouzwa ndani na nje ya nchi pamoja na kuongeza ajira zitakazoinua uchumi katika ngazi ya mtu mmoja, familia na Taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake, Meneja Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) nchini, Dkt. Patricia Laverley alisema benki hiyo inafurahi kushiriki katika miradi hiyo muhimu kwa maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
Alisema mradi wa SGR utafanikisha malengo ya kuimarisha ushirikiano wa kikanda, lakini pia kusaidia wito wa Umoja wa Afrika wa mwaka 2063 wa kuwa na Afrika iliyounganishwa, pamoja na jitihada za Afrika Mashariki za kuwa na mtandao wa reli wa kisasa utakaosaidia maendeleo katika Sekta ya madini na kilimo Tanzania.
“Zaidi ya hayo, mradi wa SGR utasaidia Serikali ya Tanzania kufikia lengo lake la kubadilisha njia ya usafirishaji kutoka barabara kwenda reli katika korido ya kiuchumi inayounga mkono Mpango wa Biashara Huria wa Bara la Afrika (ACFTA)”, alibainisha Dkt. Laverley.
Aidha, Dkt. Laverley alisema katika mkataba wa pili waliosaini wa kuongeza mtaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB), fedha zitakazotolewa zitaisaidia TADB kuongeza mnyororo mzima wa thamani wa kilimo pamoja na kusimamia biashara zinazolenga wanawake kwa kutoa mikopo kwa viwango nafuu zaidi na muda mrefu.
Naye Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Prof. Makame Mbarawa alisema reli hiyo itakayojengwa itakuwa ni kiungo muhimu cha usafirishaji kati ya bandari za Tanzania na nchi Jirani za Burundi na DRC.
Prof. Mbarawa alisema ujenzi wa kipande cha reli kutoka Uvinza hadi Musongati utatekelezwa kwa kushirikiana na Serikali ya Burundi ambapo reli ya upande wa Burundi itaanzia Malagarasi hadi Musongati na baadaye reli hiyo itafika hadi mji wa Kindu nchini DRC.
“Kukamilika kwa ujenzi wa reli ya Uvinza hadi Musongati kutawezesha kusafirisha tani milioni 3 za madini kwa mwaka kutoka mgodi mkubwa wa madini ya Nickel uliopo Musongati nchini Burundi unaokadiriwa kuwa na hifadhi ya tani milioni 150 za madini ya Nickel, Cobalt na Copper”, alibainisha Prof. Mbarawa.
Alisema kiwango cha ujenzi wa reli hiyo kitakuwa sawa na reli ya kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza, hivyo, reli hiyo itakuwa na mwendokasi wa Km 160 kwa saa kwa treni za abiria na Km 120 kwa saa kwa treni za mizigo na itakuwa na uwezo wa kubeba mizigo yenye uzito wa tani 35 kwa ekseli moja na zitakuwa zinatumia umeme.