WAZIRI wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Jerry Silaa akiwasha gari kuashiria kuanza kwa matumizi ya gari mpya kwa aijili ya Mradi wa Uboreshaji wa Miliki za ardhi (LTIP) hafla iliyofanyika leo Februari 19,2024 mji wa kiserikali Mtumba jijini Dodoma.
Na.Alex Sonna-DODOMA
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Jerry Slaa, amekabidhi magari 16 yenye thamani ya zaidi ya Sh. Bilioni 2.079 yatakayosaidia kupunguza gharama za kukodi magari wakati wa utekelezaji Mradi wa Uboreshaji wa Miliki za ardhi (LTIP).
Akizungumza katika hafla hiyo ya iliyofanyika leo Februari 19,2024 katika mji wa kiserikali Mtumba jijini Dodom,Waziri Slaa,amesema kuwa magari hayo yatasaidia kutekeleza mradi huo katika sekta ya ardhi.
Waziri Slaa amesema kuwa magari hayo 16 yatakwenda kusaidia kuharakisha utekelezaji wa mradi huo ambao umejikita katika kuboresha milki za ardhi mijini na vijijini.
“Mradi huu utakwenda kuwa suluhu kubwa katika sekta ya ardhi kwani utasaidia kupima pamoja na kupanga matumizi bora ya ardhi mijini na vijijini na kutoa hati miliki kwa wananchi”amesema Waziri Slaa
Aidha Waziri Slaa,amemuagiza mratibu wa mradi huo kuhakikisha kuwa magari hayo yanatumika kwa matumizi yaliyopangwa na sivyo vinginevyo.
‘’Magari haya yatumike kwa kazi za mradi wale wote watakao kabidhiwa magari haya wayatumie vizuri, wayatunze tusione magari haya yamebeba mkaa au kufanyika katika shughuli za harusi tungependa kuyaona yakifanya kazi ya Mradi ili mradi ukiisha tuyatumie katika wizara yetu kwenye majukumu mengine’’. amesisitiza
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga amesema thamani ya gari moja ni takribani Mil. 129.9 za Tanzania na magari hayo ni sehemu ya magari 70 yatakayonunuliwa kwa msaada wa Benki ya Dunia.
“Magari haya 16 ambayo Mweshimiwa Waziri unakabidhi ya mradi huu ni sehemu ya mengine 59 ambayo yataingia bandarini na bei ya kila gari ni Sh.milioni 129.9 na bei imeshuka kutoka na kununua kwa kutumia wakala Benki ya Dunia na mara baada ya kukabidhiwa leo hii hapa yatakwenda katika maeneo yanakohitajika”amesema Mhandisi Sanga
Mhandisi Sanga amesema kuwa Mradi huo wa uboreshani wa milki za ardhi utatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano utaogharimu zaidi ya Sh.bilioni 346 ikiwa ni mkopo kutoka benki ya Dunia (WB).
Naye Mratibu wa Mradi wa LTIP Bw. Joseph I.Shewiyo amesema magari hayo yatasaidia kwa kiasi kikubwa utekezaji wa mradi ambao umegawanyika katika sehemu kuu nnne ambazo ni Usalama wa Milki, uimarishaji mifumo ya taarifa za Ardhi na ujenzi wa miundombinu ya Ardhi.
“Kupitia mradi huu kila mmoja atakua na hati yake na hati miliki inatolewa bure mwaka huu tumepanga kufikia vijiji 700 hadi sasa tayari tumefikia vijiji 540.Pia tumepanga kufika katika mitaa 660 na halmashauri 36, lakinj pia mradi huu hadi sasa umetoa ajira kwa watu zaidi ya 700″amesema Bw.Shewiyo
WAZIRI wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Jerry Silaa akikata utepe kukabidhi magari 16 kwa aijili ya Mradi wa Uboreshaji wa Miliki za ardhi (LTIP) hafla iliyofanyika leo Februari 19,2024 mji wa kiserikali Mtumba jijini Dodoma.
WAZIRI wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Jerry Silaa akiwasha gari kuashiria kuanza kwa matumizi ya gari mpya kwa aijili ya Mradi wa Uboreshaji wa Miliki za ardhi (LTIP) hafla iliyofanyika leo Februari 19,2024 mji wa kiserikali Mtumba jijini Dodoma.
WAZIRI wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Jerry Silaa ,akimkabidhi ufunguo wa gari Katibu Mkuu Wizara wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi. Anthony Sanga kwa ajili ya kumkabidhi Mratibu wa Mradi huo.
Katibu Mkuu Wizara wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga akikabidhi ufunguo wa gari Mratibu wa Mradi huo Bw. Joseph Shewiyo kama ishara ya kuanza kutumika kwa magari hayo kwenye Mradi wa Uboreshaji wa Miliki za ardhi (LTIP) hafla iliyofanyika leo Februari 19,2024 mji wa kiserikali Mtumba jijini Dodoma.
WAZIRI wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Jerry Silaa,akizungumza mara baada ya kukabidhi magari 16 kwa aijili ya Mradi wa Uboreshaji wa Miliki za ardhi (LTIP) hafla iliyofanyika leo Februari 19,2024 mji wa kiserikali Mtumba jijini Dodoma.
KATIBU Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga,akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi magari 16 kwa aijili ya Mradi wa Uboreshaji wa Miliki za ardhi (LTIP) hafla iliyofanyika leo Februari 19,2024 mji wa kiserikali Mtumba jijini Dodoma.
Mratibu Mradi wa Uboreshaji wa Miliki za ardhi (LTIP) Bw. Joseph I.Shewiyo ,akielezea jinsi magari yatakavyotumika wakati wa hafla ya kukabidhi magari 16 kwa aijili ya Mradi wa Uboreshaji wa Miliki za ardhi
hafla iliyofanyika leo Februari 19,2024 mji wa kiserikali Mtumba jijini Dodoma.
MUONEKANO wa Magari 16 yaliyokabidhiwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Jerry Silaa kwa aijili ya Mradi wa Uboreshaji wa Miliki za ardhi (LTIP) hafla iliyofanyika leo Februari 19,2024 mji wa kiserikali Mtumba jijini Dodoma.