Kitaifa

ZABUNI ZA TACTIC KUNDI LA TATU KUTANGAZWA MWISHONI MWA FEBRUARI,2024

Written by mzalendo

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Deogratius Ndejembi amesema Zabuni za kupata wasanifu wa kundi la tatu lenye miji 18 ikiwemo Halmashauri ya Mji wa Tunduma zitatangazwa mwishoni mwa mwezi huu wa Februari 2024.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Deogratius Ndejembi wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe, Mhe Juliana Shonza aliyetaka kujua ni lini utekelezaji wa mradi w TACTIC katika Mji wa Tunduma utaanza.

“ Zabuni za kuwapata wasanifu wa kundi la tatu zitatangazwa Februari mwaka huu na wasanifu watakaopatikana watasaini mikataba Juni 2024 kwa mikataba ya usanifu kwa miezi nane.

Baada ya kukamilisha usanifu, zabuni za kuwapata wakandarasi na washauri elekezi kwa pamoja zitatangazwa mwezi April 2025,” Amesema Mhe Ndejembi.

Mradi wa TACTIC unahusu uboreshaji wa miundombini ya miji 45 kufuatia Benki ya Dunia kutoa Dola za Kimarekani Milioni 410 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo.

About the author

mzalendo