Kimataifa

AUAWA WAKATI MABINGWA WA SUPER BOWL, CHIEFS WAKISHEREKEA USHINDI

Written by mzalendo

Msururu wa ufyatuaji wa risasi uliua mtu mmoja na kujeruhi wengine 21 Jumatano nje ya kituo kikuu cha reli katika mji wa Kansas, jimbo la Missouri, hapa Marekani, ambapo mabingwa wa mwaka huu wa mashindano ya mpira wa miguu Marekani (NFL), Chiefs, walikuwa wakisherekea ushindi wao wa Super Bowl.

Mkuu wa polisi Stacey Graves aliuambia mkutano wa waandishi wa habari kwamba washukiwa wawili wako chini ya ulinzi.

Awali, polisi walisema washukiwa hao walikuwa na silaha. Alisema mtu mmoja aliuawa na wengine kati ya 10 na 15 walijeruhiwa na risasi.

Wachezaji wote wa Chiefs, makocha na wasaidizi ambao walishiriki hafla hiyo ya kusherekea ushindi wako salama, Meya wa Kansas Quinton Lucas aliwambia waandishi wa habari.

Watu watatu wamekamatwa kufuatia shambulizi hilo.

About the author

mzalendo