Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama akitoa ufafanuzi kuhusu hoja za wabunge zilizowasilishwa wakati wa majadiliano ya miswada ya sheria ya uchaguzi katika Bunge linaloendelea Jijini Dodoma tarehe 02, 2024.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Ummy Nderianana akichangia maoni yake kuhusu miswada ya sheria ya uchaguzi wakati wa Bunge linaloendelea Jijini Dodoma tarehe 02 Februari, 2024.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha muswada wa sheria ya Tume ya Taifa ya uchaguzi, muswada wa sheria ya uchaguzi wa Rais, wabunge na madiwani na muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa.
Miswada hiyo mitatu imepitishwa mara baada ya kujadiliwa na wabunge katika mkutano wa 14 wa Bunge linaloendelea Jijini Dodoma Februari 02, 2024 ambapo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama alitoa ufafanuzi kuhusu hoja za wabunge zilizowasilishwa wakati wa majadiliano ya miswada ya sheria ya uchaguzi.