Uncategorized

MIL. 180 ZAKARABATI SHULE CHAKAVU KIBITI’ NDEJEMBI

Written by mzalendo

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe Deogratius Ndejembi amesema katika mwaka wa fedha 2023/24, Serikali imepeleka Sh Milioni 180 kwa ajili ya ukarabati wa shule chakavu za msingi katika Jimbo la Kibiti mkoani Pwani ambapo jumla ya shule nne zitakarabatiwa ambazo ni Pongwe (Madarasa Matatu), Mchinga (Madarasa Mawili), Saninga (Madarasa Mawili) na Misimbo (Madarasa Mawili).

Mhe Ndejembi ameyasema hayo leo Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Kibiti, Mhe Twaha Mpembenwe aliyehoji ni lini Serikali itaanza ukarabati wa Shule Chakavu za Msingi Jimbo la Kibiti.

About the author

mzalendo