Serikali inatarajia kutumia zaidi ya shilingi bilioni 899 kufundisha na kuwalipa posho ya kila mwezi wahudumu wa afya ngazi ya jamii wapatao laki 137,294 ili kutoa elimu ya afya, Lishe na kupinga ukatili wa kijinsia kwenye jamii.

Hayo yamebainishwa leo Januari 31, 2024 na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel wakati akijibu swali namba 34 kutoka kwa Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Tamima Haji Abas kwa niaba ya Waziri wa afya Mhe. Ummy Mwalimu ambapo swali linasema Je, kuna mpango gani wa kutayarisha vipindi vya elimu vya kupinga ukatili wa kijinsia katika Kliniki za Mama na Mtoto Nchini.

Wahudumu hawa watakuwa wawili kwa kila Mtaa (Mitaa yote 4,263) na wawili kwa kila kitongoji (Vitongoji 64,384) ili kutoa elimu ya afya, lishe na kupinga ukatili wa kijinsia.

“Ni wazo zuri sana kutoa elimu ya kupinga ukatili wa kijinsia katika kliniki za Mama na Mtoto na Serikali imekwisha anza mkakati huo ambao sio tu kwenye kliniki lakini pia kwa kupitia vipindi vya luninga na redio”, ameeleza Dkt. Mollel.

Dkt. Mollel ameongeza kuwa mkakati huo unazinduliwa leo tarehe 31 Januari, 2024 na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. Philip Isdory Mpango.

Previous articleSERIKALI YAANZA KUFANYA TATHMINI KUBAINISHA MAENEO YANAYOHITAJI MABORESHO KUKABILIANA NA ATHARI ZA MAZINGIRA
Next articleUTUNZAJI KUMBUKUMBU KURAHISISHA MALIPO YA BIMA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here