Na Gideon Gregory, Dodoma.
Jumla ya watoto watatu waliofanyiwa huduma upandikizaji wa uloto kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa wamepona ugonjwa wa seli mundu kwa kupandikizwa uloto tangu huduma hiyo ianze kutolea Januari 19,2023 ambapo watoto hao wote walifanyiwa kwa hawamu moja kwa mara ya kwanza.

Hayo yamebainishwa leo January 30, 2024 Jijini Dodoma na Mkurugenzi mtendaji wa hospitali hiyo Dkt. Alphonce Chandika wakati akizungumza na wanahabari kuhusiana na mwaka mmoja wa mafanikio waliyoyapata tangu kuanza kutoa huduma.

“Siku ya leo ni muhimu kwetu kwasababu tumefanikiwa kuwasaidia watoto hawa pia tunawashukuru wazazi na walezi wa watoto hao kwa kutuamini, kwasababu sauala hili halikuwa rahisi katika kulifanikisha,” amesema.

Dkt. Chandika ameongeza kuwa kwa mwaka jumla ya watoto 11,000 uzaliwa kwa mwaka wakiwa na ugonjwa huo na kuongeza kuwa duniania Tanzania inashika nafasi ya nne na Afrika ya tatu kwa nchi zenye tatizo hilo.

“Hii inaonesha kuwa ugonjwa huu nchini bado ni kubwa lakini tunafahamu kwamba watoto wanaozaliwa na ugonjwa huu ambao ni takribani 11,000 kwa mwaka wengi wao hawafikii miaka mitano zaidi ya 50% upoteza maisha na wanao weza kuishi zaidi au kuvuka miaka mitano wengi wao wanaishi kwa takribani miaka 45,” amesema.

Kwa upande wake daktari wa magonjwa yad amu na saratani kwa watoto Dkt. Shakilu Jumanne amezungumzia kuhusu matibabu ya ugonjwa huo ambapo amesema kuwa dawa za kupunguza makali ufanya kazi japo haziwezi kusaidia kwa watoto wengi kulingana na hali ya ugonjwa alionao.

“Kwahiyo kigezo cha kwanza kwa mtu anayetaka kupandikizwa uloto lazima awe ametumia dawa hizo lakini hazijaleta matokeo yoyote hivyo tunatumia hicho kama kigezo cha kwanza katika kumuhudumia,” amesema.

Akizungumza kwa niaba ya watoto wenzake ambao wamefanyiwa upandikizaji huo Elisha Joseph amesema changamoto kubwa ambayo alikuwa akiipitia kipindi anasumbuliwa na seli mundu kupitia maumivu makali ikiwemo tumbo kuuma.

Previous articleTANZANIA YAPOKEA MSAADA WA Sh. TRIL 1.4 KUTOKA GLOBAL FUND
Next articleDKT.DUGANGE:VIKUNDI 345 VIMEKIDHI VIGEZO VYA KUPEWA ZABUNI

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here