Featured Kitaifa

RAIS SAMIA AZINDUA UGAWAJI WA VIZIMBA VYA KUFUGIA SAMAKI NA BOTI ZA KISASA KWA AJILI YA WAVUVI WA KANDA YA ZIWA, JIJINI MWANZA

Written by mzalendo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria uzinduzi wa ugawaji wa vizimba vya kufugia Samaki na Boti za Kisasa kwa ajili ya Wavuvi wa Kanda ya Ziwa kwenye hafla fupi iliyofanyika pembezoni mwa Ziwa Victoria (Bismarck Rock) Jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024. Wengine katika picha ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega, Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Emanuel Nchimbi, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Amos Makalla, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Profesa Riziki Shemdoe pamoja na viongozi wengine.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Amos Makalla mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Mwanza kwa ajili ya ziara ya Kikazi ya siku moja tarehe 30 Januari, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Emmanuel Nchimbi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Mwanza kwa ajili ya ziara ya Kikazi ya siku moja mkoani humo tarehe 30 Januari, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega kuhusu Boti za Kisasa na vizimba vya kufugia Samaki kwa ajili ya Wavuvi wa Kanda ya Ziwa kwenye hafla fupi iliyofanyika pembezoni mwa Ziwa Victoria (Bismarck Rock) Jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na baadhi ya Wabunge wa Mkoa wa Mwanza mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Mwanza kwa ajili ya ziara ya Kikazi ya siku moja mkoani humo tarehe 30 Januari, 2024.

Baadhi ya Machifu wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa wakiwa kwenye mkutano wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan uliofanyika kwenye uwanja wa Nyamagana tarehe 30 Januari, 2024.

Muonekano wa Boti za Kisasa pamoja na vizimba vya kufugia Samaki ambavyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amezindua ugawaji wake kwa ajili ya Wavuvi wa Kanda ya Ziwa kwenye hafla iliyofanyika Jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024. Boti na vizimba hivyo vimegaiwa kwa Wavuvi kwa mkopo usio na riba ili kuwawezesha kufanya Biashara ya Samaki kwa tija.

Baadhi ya Viongozi wa dini pamoja na wananchi wakiwa kwenye mkutano wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan uliofanyika kwenye uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akibonyeza Kitufe kuzindua ugawaji wa vizimba vya kufugia Samaki na Boti za Kisasa kwa ajili ya Wavuvi wa Kanda ya Ziwa kwenye hafla fupi iliyofanyika pembezoni mwa Ziwa Victoria (Bismarck Rock) Jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega wakati akielekea kuzindua Zoezi la ugawaji wa vizimba vya kufugia Samaki na Boti za Kisasa kwa ajili ya Wavuvi wa Kanda ya Ziwa kwenye hafla fupi iliyofanyika pembezoni mwa Ziwa Victoria (Bismarck Rock) Jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Mwanza kwa ajili ya ziara ya Kikazi ya siku moja mkoani humo tarehe 30 Januari, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiangalia vikundi vya ngoma Chapakazi kutoka Ilemela na Buyegi kutoka Kisesa Magu mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa Mwanza kwa ajili ya ziara ya Kikazi ya siku moja mkoani humo tarehe 30 Januari, 2024.


Msanii Mrisho Mpoto akitumbuiza kwenye hafla ya uzinduzi na ugawaji wa Boti za Kisasa na vizimba kwa ajili ya Wavuvi wa Kanda ya Ziwa iliyofanyika katika uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega wakati akielezea kuhusu Samaki wa aina mbalimbali wanaopatikana katika Ziwa Victoria mara baada ya uzinduzi wa boti za kisasa pamoja na vizimba vya kufugia Samaki Jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024.

Msanii Dullah Makabila akitumbuiza kwenye hafla ya uzinduzi na ugawaji wa Boti za Kisasa na vizimba kwa ajili ya Wavuvi wa Kanda ya Ziwa uliofanyika katika uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Mkoa wa Mwanza mara baada ya uzinduzi wa ugawaji wa Boti za Kisasa na vizimba kwa ajili ya Wavuvi wa Kanda ya Ziwa katika uwanja wa Nyamagana Jijini Mwanza tarehe 30 Januari, 2024.

About the author

mzalendo