Featured Kitaifa

LSF NA NMB FOUNDATION YAINGIA MAKUBALIANO YA KUWAWEZESHA WANAWAKE NA WASICHANA KIJAMII NA KIUCHUMI

Written by mzalendoeditor
 
 
Shirika lisilo la Kiserikali la LSF na NMB Foundation yamesaini makubalinao ya mashirikiano kwa lengo la kutekeleza kwa pamoja miradi ya kijamii yenye lenye lengo la kuwainua wanawake na wasichana kijamii na kiuchumi .Mashirikiano haya yamesainiwa leo katika ukumbi wa mikutano wa benki ya NMB, na yanategemewa kuwa makubaliano ya muda wa miaka mitatu. 
Makubaliano hayo yamelenga kutekeleza miradi iliyo katika sekta za Elimu, Ujasiriamali, Afya na Mazingira maeneo ambayo mashirika haya yamekuwa yakitekeleza miradi yake Kupitia makubaliano haya LSF na NMB Foundation zimelenga kuweka nguvu ya pamoja katika kutafuta rasilimali fedha za pamoja katika kutekeleza miradi mbalimbali nchini 
 
Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2021 NMB foundation imekuwa ikitekeleza miradi yake katika sekta hizi muhimu za Elimu, Afya, Kilimo, Mazingira na Ujasiriamali. Kwa lengo la kukuza ujumuishaji endelevu na wa kiuchumi. Aidha LSF imejikita katika kuhakikisha haki ya wanawake kijamii na kiuchumi zinafikiwa nchi nzima kwa kutoa elimu na kuwajengea uwezo jamii, kuhakikisha usawa na fulsa mbalimbali zinapatikana kwa wote ikiwemo elimu, afya bora, mazingira safi, na rasilimali kwa kutekeleza miradi ya jamii katika kata na wilaya Tanzania bara na Zanzibar 
 
Makubalino haya kati ya LSF na NMB foundation yanakuja katika kipindi ambacho nchi yetu inatekeleza agenda ya kuinua wanawake kiuchumi na kupiga hatua katika kufikaia malengo ya Dira ya Maendeleo ya Kitiafa ya mwaka 2025 na malengo ya SDG ifikapo 2030. Hivyo mashirikiano haya yamelenga kuchangia katika kufikia malengo haya. Akiongea wakati wa utiaji Saini wa makubaliano haya, Bw. Nelson Karumuna, Meneja Mkuu wa NMB Foundation, alielezea shauku yake kuhusu ushirikiano huo, akisema, “Kama taasisi 
 
inayotekeleza miradi ya kijamii, NMB Foundation inategemea makubwa sana kutokana na mashirikiano haya. Huu ni ushirikiano kati ya taasisi mbili zenye ushawishi katika maeneo yake ya kiutendaji. Sisi tupo zaidi katika sekta ambayo tunaweza kushirikiana na Taasisi ya LSF katika kuwawezesha wanawake na wasichana kijamii na kiuchimi. Hivyo ni mategemeo yetu kuwa kuunganishwa kwa nguvu zetu kwa Pamoja kutawezesha miradi mingi kuanzishwa na kuwafikia watanzania wengi zaidi Tanzania Bara na Zanzibar. Tumejiwekea lengo la kuwekeza nguvu katika kutafuta rasilimali fedha kwa pamoja kutoka katika vyanzo mbalimbali vya ndani na nje kwa muda wa miaka mitatu Alisema Bw. Karumuna. 
 
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa LSF , Bi Lulu Ng’wanakilala alisema” Tunajisikia fahari kuingia makubaliano na sekta binafsi na tunafurahi kuona Sekta binafsi kama NMB Foundation inakuwa mstari wa mbele katika kuibua mbinu mbadala za mashirikiano yenye tija katika kutatua changamoto za kijamii na NMB Foundation ni mfano Dhahiri leo. Sisi LSF kwa takribani miaka 12 tumekuwa tukitekeleza miradi yetu katika ngazi za jamii na bado tumeona kuna changamoto kubwa katika kuwawezesha wanawake na watoto wakike kielimu, kiafya, kiuchumi hivyo ushirikiano tunaoanzisha leo na NMB foundation yataleta tija katika kuchangia kutatua changamoto hizi. 
 
LSF tunaamini kwa wadau kuungana na kuweka nguvu ya pamoja na hivyo tumekuwa tukifanya kazi kwa karibu na Serikali na taasisi zake, wadau wa maendeleo, mashirika yasiyo ya kiserikali, sekta binafsi hivyo kusaini makubaliano haya na NMB foundation leo ni hatua kubwa katika kufanya program zetu kuwa endelevu.Ni dhahiri kwamba mashirikiano haya yalioingiawa leo kati ya Taasisi hizi mbili yatakua na tija katika kuongeza nguvu za pamoja na kuweka rasilimali za pamoja katika kuchangia kutokomeza umasikini, kutokomeza tofauti za kijinsia, na kukuza ukuaji wa kiuchumi unaowajumuisha watu wote nchini Tanzania hususani wanawake na wasichana ambao wamekuwa wakiachwa nyuma. aliongeza Ng’wanakilala 
 
LSF na NMB Foundation zinaamini katika mashirikiano kama chachu ya kuleta maendeleo endelevu katika jamii. Makubaliano haya ni mwanzo wa utekelezaji wa miradi yenye lengo la kuendelea kuzikifikia jamii na vikundi mbalimbali vyenye uhitaji Tanzania Bara na Zanzibar. 
 
LSF na NMB Foundation wamesaini makubaliano ya ushirikiano kwa lengo la kutekeleza kwa pamoja miradi ya kijamii yenye lengo la kuwainua wanawake na watoto wa kike kijamii na kiuchumi. Makubaliano hayo yamelenga kutekeleza miradi iliyo katika sekta za Elimu, Ujasiriamali, Afya na Mazingira, maeneo ambayo mashirika haya yamekuwa yakitekeleza miradi yake. Mkataba huo umesainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa LSF, Lulu Ng’wanakilala, na Meneja Mkuu wa NMB Foundation, Nelson Karumuna
 
Mkurugenzi Mtendaji wa LSF, Lulu Ng’wanakilala, na Meneja Mkuu wa NMB Foundation, Nelson Karumuna, wakibadilishana mikataba ya makubaliano ya ushirikiano ya miaka mitatu yatawawezesha kushirikiana katika kutafuta rasilimali na kutekeleza miradi ya pamoja katika sekta za elimu, afya, ujasiriamali, na mazingira.
 
Tumejipanga kuwawezesha wanawake kijamii na kiuchumi , Mkurugenzi Mtendaji wa LSF, Lulu Ng’wanakilala, na Meneja Mkuu wa NMB Foundation, Nelson Karumuna katika picha mara baada ya kusaini makubaliano

About the author

mzalendoeditor