Featured Kitaifa

TUSHIRIKIANE KUDHIBITI ATHARI ZA KIAFYA ZINAZOTOKANA NA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI.

Written by mzalendo

Na WAF Geneva, Uswisi

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. John Jingu ametoa wito kwa Shirika la Afya Duniani WHO kushirikiana na kujenga uwezo kwa nchi wanachama katika kudhibiti athari za kiafya na magonjwa yanayotokana na mabadiliko tabia nchi.

Dkt. Jingu amesema hayo jana Januari 22, 2024 akiwa kwenye Mkutano wa 154 wa Bodi ya Shirika la Afya Duniani unaoendela kufanyika katika Makao Makuu ya WHO Jijini Geneva, Uswisi.

Amesema kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizoathirika sana na madabiliko ya tabia ya nchini hivyo kusababisha majanga ikiwemo mafuriko na ukame ikiwa ni majanga ambayo huwa yanasababisha madhara ya afya kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

“Tunaliomba Shirika la Afya Duniani kuongezea uwezo kwa nchi wananchama wa WHO katika kushughulikia athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia ya nchi” amesema Dkt. Jingu.

Katika hatua nyingine Dkt. Jingu ameishukuru WHO kupitia Mkurugenzi Mkuu wa Shirikila hilo Dkt Tedros Gebreyesus, kwa kushirikiana na Tanzania kuweza kuudhibiti ugonjwa wa Marburg nchini Tanzania ndani ya muda mfupi pamoja na ushirikiano wa karibu ambao WHO inautoa kwa Tanzania katika kudhibiti magonjwa ya mlipuko ikiwemo UVIKO-19.

About the author

mzalendo