Kitaifa

WAZIRI MCHENGERWA AKUTANA NA MKURUGENZI MKAAZI WA USAID

Written by mzalendo

OR- TAMISEMI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa amekutana na kuzungumza na Mkurugenzi Mkazi ‘Mission Director” wa Shirika la Misaada la Watu wa Marekani (USAID), Craig Hart kwenye Ofisi ndogo za Wizara zilizopo magogoni kwake jijini Dar es salaam leo tarehe 22.01.2024.

Mazungumzo hayo yalilenga kuendeleza mashirikiano katika kuboresha huduma za Afya msingi hususan kuongeza wigo wa utekelezaji wa miradi ya USAID kwenye maeneo mengi zaidi, kuongeza idadi ya watumishi wa Afya, kutoa mafunzo na motisha kwa wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii.

Aidha kuendelea kusaidia Mpango wa Usafirishaji/Rufaa za Dharura kwa Mama wajawazito na watoto wachanga kupitia Madereva wa Magari madogo Ngazi ya Jamii, Kuimarisha Mifumo ya Afya ngazi ya Huduma ya Afya ya Msingi pamoja na ukarabati wa miundombinu ya kutolea huduma za Afya na ununuzi wa vifaz na vifaatiba.

Katika eneo la Elimu maeneo ya mashirikiano yaliyojadiliwa zaidi ni kuona namna ya kuongeza idadi ya walimu wa kujitolea wanaokuja kufundisha shule za Sekobdari ( Peace Coprs) ambapo kwa mwaka huu waliokuja nchini ni 35 tu. Walimu hao wanahitajika zaidi kwa ajili ya masomo ya Sayansi, Uhandisi, ICT, Englisha na Hesabu.

Na Kupitia mradi wa Jifunze Uelewe unaotekelezwa kwa fedha kutoka USAID ofisi ya Rais – TAMISEMI imeomba mradi huu uweze pia kujenga na miundombinu ya shule kwenye mikoa unapotekelezwa!

Waziri Mchengerwa ameahidi ushirikiano wa kutosha kwa Uongozi wa Shirika hilo na kumkaribisha Mkurugenzi huyo kufanya kazi zaidi katika maeneo mengine yanayosimamiwa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI

Ziara ya Mkurugenzi Mkaazi wa USAID Craig Hart ilikuwa na lengo la kujitambusha na kuona namna Shirika hilo linavyoweza kushirikiana zaidi na OR-TAMISEMI.

About the author

mzalendo