Kitaifa

MHE. LONDO APOKEA TAARIFA YA OR-TAMISEMI

Written by mzalendo

MWENYEKITI wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe Denis Londo leo ameongoza kamati hiyo kupokea na kujadili taarifa ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI, kuhusu usimamizi na uendeshaji wa Sekretarieti za Mikoa: Mafanikio, Changamoto na hatua za utatuzi.

Kikao hicho pia kimepokea na kujadili taarifa ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI kuhusu usimamizi na uendeshaji wa Halmashauri za Serikali za Mitaa: Mafanikio, Changamoto na Hatua za utatuzi.

Pia kamati imepokea na kujadili taarifa ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI kuhusu usimamizi wa shughuli za ujenzi wa miundo ya barabara wa kawaida na wakati wa dharura chini ya mamlaka za serikali za mitaa.

Kikao hicho kimefanyika leo katika kumbi za Bunge jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Adolf Ndunguru na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI anayeshughulikia miundombinu, Mhandisi Rogatus Mativila.

About the author

mzalendo