Kitaifa

KATIBU MKUU MPYA WA CCM BALOZI MSTAAFU DKT EMMANUEL NCHIMBI APOKELEWA KWA SHANGWE NA MAMIA YA WANA- CCM MKOA WA DAR ES SALAAM

Written by mzalendo
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Dkt. Emmanuel John Nchimbi akilakiwa na Viongozi na wanachama wa CCM Mkoa wa Dar Es Salaam alipowasili katika Viwanja Vya Mnazi Mmoja kuzungumza na Wanachama wa CCM Mkoani humo.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Dkt. Emmanuel John Nchimbi, Akihutubia wana-CCM wa Dar es salaam baada ya kupokelewa kwa nderemo na vifijo katika Viwanja Vya Mnazi Mmoja, Jijini Dar Es Salaam Leo Januari 20, 2024.( Picha na Fahadi Siraji wa CCM).
Wanachama na Viongozi waliowasili Kumlaki Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Dkt. Emmanuel John Nchimbi wakifuatilia Mkutano.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Dkt. Emmanuel John Nchimbi, akizungumza na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Ndg. Anamringi Macha katika Viwanja Vya Mnazi Mmoja kuzungumza na Wanachama wa CCM Mkoani humo.

About the author

mzalendo