Na Mwandishi Wetu, Dodoma.
Afisa elimu wa mkoa wa Dodoma Mwl. Vicent Kayombo ametoa taarifa kwa umma juu ya ripoti ya tarehe 17 January 2024 ya wanafunzi walioandikishwa shuleni mkoani Dodoma ndani ya mwaka 2024.
Mwl. Kayombo ameyasema hayo leo Januari 17,2024 alipotoa taarifa juu ya wanafunzi wa elimu ya awali walioripoti mashuleni kufikia asilimia 84.56 ya wanafunzi wote waliokuwa wameandikishwa kuanza masomo yao.
Amesema jumla ya wanafunzi 55,364 wameweza kuripoti shuleni na kati ya wanafunzi 65,471 ambayo ni sawa na asilimia 74.56 kwenye elimu ya awali huku kwa darasa la kwanza wameweza kufikia asilimia 88.88 ya wanafunzi wote ambao waliokuwa wameandikishwa shuleni.
“Jumla ya wanafunzi 71,536 wamerioti shuleni na kati ya wanafunzi 80,482 waliotakiwa kuripoti shuleni kwaio hiyo ni sawa na asilimia 88.88, lakini kwa kidato cha kwanza mkoa umefanikiwa kufikia asilimia 57.31 na hapa jumla ya wanafunzi 30,306 wameweza kuripoti shuleni kati ya wanafunzi 52,880 ambao wamepangwa kwenye shule zetu za mkoa wa Dodoma”.
“Mhe. mkuu wa mkoa amekuwa akitoa maelekezo kwa viongozi wote ndani ya mkoa kuendelea kufanya uhamasishaji kwenye ngazi zao kuhakikisha kwamba wanafunzi wote ambao wana umri wa kwenda shule ambao wameandikishwa wote wanaripoti shuleni”,amesema mwl. Kayombo.
Aidha ameongezea kuwa mkuu wa mkoa mhe. Rosemary Senyamule amekuwa akizunguka kuongea na wananchi anapokagua miradi katika halmashauri zote na kupitia mikutano hiyo amekuwa akihamasisha wazazi kuhakikisha wanawapeleka watoto wao shuleni na pia maelekezo yametoka kwa watendaji wa vijiji na wa kata kupita nyumba hadi nyumba kuhakikisha watoto wote ambao wamefauru wanakwenda shuleni.
Pia ameongezea kuwa ni jukumu la wazazi kumuunga mkono mhe. Rais kupeleka watoto shuleni kwani amefanya uwekezaji mkubwa kwenye eneo la elimu kwa kujenga majengo ya shule za sekondari kupitia mradi wa SEQUIP na sasa kuna shule mpya 14 ambazo tiyari zimepokea wanafunzi.
“Mhe. mkuu wa mkoa ametoa maelekezo kuwa wanafunzi wote waliochaguliwa waende shuleni bila kujali mwanafunzi ana sare au hana sare ya shule ila awe tu na vifaa vya kuandikia pamoja na daftari na sare za shule zitamfuata mtoto akiwa masomoni.
Sambamba na hayo Mwl. Kayombo ametoa rai kwa wazazi na walezi wote wa mkoa wa Dodoma kuhakikisha watoto wao wana hudhuria shuleni kila siku tangu siku anayoanza shule na kuendelea kusimamia mahudhurio ya watoto wao mashuleni.