Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango akishiriki ufunguzi wa Mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF) unaofanyika Davos nchini Uswisi. Tarehe 16 Januari 2024
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango, leo tarehe 16 Januari 2024 ameshiriki ufunguzi wa Mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani (World Economic Forum 2024) linalofanyika Davos nchini Uswisi.
Makamu wa Rais anamwakillisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano huo unaolenga kujadili masuala mbalimbali ikiwemo uchumi na uwekezaji, utawala bora, usalama wa chakula, mabadiliko ya tabia ya nchi pamoja na kilimo.
Mkutano huo umefunguliwa na Rais na Mwanzilishi wa Jukwaa hilo Prof. Klaus Schwab ukifuatiwa na hotuba kutoka kwa Rais wa Uswisi Mhe. Viola Amherd.
Mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani unahudhuriwa na Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka mataifa mbalimbali, Watendaji Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa, Wakuu wa Taasisi na Makampuni mbalimbali duniani pamoja na Wafanyabiashara.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango akishiriki ufunguzi wa Mkutano wa Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF) unaofanyika Davos nchini Uswisi. Tarehe 16 Januari 2024.