Featured Kitaifa

WORLD VISION TANZANIA YAJITOSA KUPAMBANA NA KIPINDUPINDU SHINYANGA

Written by mzalendoeditor
Kaimu Meneja wa Shirika la World Vision Kanda ya Ziwa Bi. Irene Abusheikh (katikati) akikabidhi vifaa tiba na vifaa kinga kwa Kaimu Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga Rad. Faustine Mulyutu ili kusaidia utoaji huduma kwenye kupambana na mlipuko wa Kipindupindu Mkoani Shinyanga. Wa kwanza kushoto ni Mhasibu Mkuu wa World Vision Kanda ya Ziwa Bw. Lukelo Kivambe

 

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
 
Shirika la World Vision Tanzania limetoa msaada wa vifaa tiba, vifaa kinga na dawa za kutibu visima vya maji vyenye thamani ya shilingi Milioni 7 (Tsh. 7,059,080/=) ili kusaidia utoaji huduma kwenye kupambana na mlipuko wa Kipindupindu Mkoani Shinyanga.
 
 
Akikabidhi vifaa hivyo leo Alhamisi Januari 11,2024, Kaimu Meneja wa Shirika la World Vision Kanda ya Ziwa Bi. Irene Abusheikh amesema vifaa hivyo vitasaidia utoaji huduma katika mapambano ya ugonjwa wa kipindupindu.
 
“Shirika la World Vision Tanzania linashirikiana na serikali na wadau wengine katika ngazi zote kuboresha mfumo na huduma za afya katika nchi yetu, hivyo tunatoa vifaa tiba na dawa vyenye thamani ya shilingi 7,059,080/= ikiwa ni sehemu ya kuchukua hatua dhidi ya mlipuko wa Kipindupindu katika Mkoa wa Shinyanga vitakavyosaidia utoaji huduma kwenye kupambana na Kipindupindu kwenye vituo vilivyowekwa kuhudumia wagonjwa pamoja na kuzuia maambukizi zaidi”,amesema Abusheikh.
Miongoni mwa vifaa vilivyotolewa ni pamoja na Chroline tablets, Dettol,Savlon,Examination gloves, theatre boots, tab Zinc sulphate, Ringer’s Lactate na ORS.
 
Akipokea vifaa hivyo, Kaimu Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga Rad. Faustine Mulyutu ameishukuru World Vision Tanzania kwa msaada huo ambao utasaidia sana katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa kuhara na kutapika.
 
 
“Tunawashukuru wadau wetu World Vision Tanzania kwa kukubali kuitika kwa haraka baada ya kupokea maelekezo kutoka kwa Mheshimiwa Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwamba wadau washirikiane na serikali bega kwa bega katika kupambana na janga hili ambapo wananchi wetu wana changamoto ya kutapika na kuharisha katika Halmashauri ya wilaya ya Kishapu na Manispaa ya Kahama”,amesema Rad. Mulyutu.
Kaimu Meneja wa Shirika la World Vision Kanda ya Ziwa Bi. Irene Abusheikh (katikati) akikabidhi vifaa tiba na vifaa kinga kwa Kaimu Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga Rad. Faustine Mulyutu.
 
“Msaada huu utaenda kusaidia kiasi kikubwa sana kwa wananchi wetu waliopo kwenye kambi za matibabu pale Kagongwa na kituo cha afya Kishapu. Tumepokea madawa tiba , vifaa kinga pamoja madawa mengine ya kwenda kutibu visima ambavyo mara nyingi vinakuwa vyanzo vya vimelea kwa wananchi wetu ambao hawana maji safi na salama”,ameongeza Rad. Mulutyu.
 
 
Katika hatua nyingine amesema idadi ya wagonjwa wanaokabiliwa na changamoto ya kuhara na kutapika imeongezeka kutoka 41 hadi 57 ambapo kati yao 34 wamepatiwa huduma za matibabu na kuruhusiwa kutoka, waliopo kwenye vituo vya Kagongwa na Kishapu ni 18 wanaendelea kupatiwa matibabu.
 
“Kuna ongezeko la wagonjwa 16 wanaokabiliwa na changamoto ya kuharisha na kutapika, hakuna kifo kilichotokea, wagonjwa 34 wameruhusiwa kutoka, 18 tunaendelea kuwapatia matibabu ambapo kati ya hawa 18 , wagonjwa 8 wamechukuliwa vipimo vya awali vya Kipindupindu na hao wengine wao wanakabiliwa tu na changamoto ya kuhara na kutapika”,ameeleza Rad. Mulyutu.
 
 
Aidha amesema tayari wameanza kugawa dawa (Aqwa tab) kwa wananchi kwa ajili ya kutibu maji kwenye visima na vyombo vya kuhifadhia maji yakiwemo matanki ili kuua vimelea vinavyosababisha ugonjwa wa kuhara na kutapika ambapo mwitikio wa wananchi ni mkubwa.
 
Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza na waandishi wa habari Januari 9,2024,  alisema watu 18 kati ya 41 ambao walikabiliwa na tatizo la kuhara na kutapika hadi Januari 9,2024 walibainika kuwa na ugonjwa wa kipindupindu mkoani Shinyanga.
 
 
Alisema tangu kuanza mlipuko wa ugonjwa huo wa kuhara na kutapika, wagonjwa waliobainika ni 41 na 18 kati yao wamethibitika kuwa na ugonjwa wa Kipindupindu baada ya vipimo vya kitaalamu kufanyika.
 
 
Alisema ugonjwa wa kuhara na kutapika umesababisha vifo vya watu watano katika kata ya Kagongwa halmashauri ya Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga tangu ugonjwa huo ulipozuka mnamo tarehe 28 Desemba mwaka 2023 katika kata hiyo.
 
 
“Jumla ya vifo vitano vimetoka kwenye jamii na kifo kimoja kimetokea kwenye zahanati binafsi na wote hawa hawakufanyiwa vipimo vya kuthibitika wamekufa na ugonjwa gani hivyo Vifo vya watu hao watano haikubainika moja kwa moja kwamba walikufa kwa kipindupindu”,alisema Mndeme.
Kaimu Meneja wa Shirika la World Vision Kanda ya Ziwa Bi. Irene Abusheikh akizungumza wakati akikabidhi vifaa tiba na vifaa kinga ili kusaidia utoaji huduma kwenye kupambana na mlipuko wa Kipindupindu Mkoani Shinyanga leo Alhamisi Januari 11,2024 – Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Kaimu Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga Rad. Faustine Mulyutu akizungumza wakati akipokea vifaa tiba na vifaa kinga kutoka World Vision Tanzania.
Kaimu Meneja wa Shirika la World Vision Kanda ya Ziwa Bi. Irene Abusheikh (katikati) akikabidhi vifaa tiba na vifaa kinga kwa Kaimu Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga Rad. Faustine Mulyutu (kulia) ili kusaidia utoaji huduma kwenye kupambana na mlipuko wa Kipindupindu Mkoani Shinyanga. Wa kwanza kushoto ni Mhasibu Mkuu wa World Vision Kanda ya Ziwa Bw. Lukelo Kivambe
Kaimu Meneja wa Shirika la World Vision Kanda ya Ziwa Bi. Irene Abusheikh (katikati) akikabidhi vifaa tiba na vifaa kinga kwa Kaimu Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga Rad. Faustine Mulyutu ili kusaidia utoaji huduma kwenye kupambana na mlipuko wa Kipindupindu Mkoani Shinyanga. Wa kwanza kushoto ni Mhasibu Mkuu wa World Vision Kanda ya Ziwa Bw. Lukelo Kivambe
Kaimu Meneja wa Shirika la World Vision Kanda ya Ziwa Bi. Irene Abusheikh (kushoto) na Mhasibu Mkuu wa World Vision Kanda ya Ziwa Bw. Lukelo Kivambe wakikabidhi nyaraka za vifaa tiba na vifaa kinga kwa Kaimu Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga Rad. Faustine Mulyutu 
Kaimu Meneja wa Shirika la World Vision Kanda ya Ziwa Bi. Irene Abusheikh (kushoto) na Mhasibu Mkuu wa World Vision Kanda ya Ziwa Bw. Lukelo Kivambe wakikabidhi nyaraka za vifaa tiba na vifaa kinga kwa Kaimu Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga Rad. Faustine Mulyutu 
 Kaimu Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga Rad. Faustine Mulyutu akikagua vifaa tiba na kinga vilivyotolewa na World Vision Tanzania. Kushoto ni Mhasibu Mkuu wa World Vision Kanda ya Ziwa Bw. Lukelo Kivambe
Kaimu Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga Rad. Faustine Mulyutu (kulia) akisaini nyaraka za vifaa tiba na kinga vilivyotolewa na World Vision Tanzania. Kulia ni Kaimu Meneja wa Shirika la World Vision Kanda ya Ziwa Bi. Irene Abusheikh
Muonekano wa sehemu ya vifaa tiba na vifaa kinga vilivyotolewa na World Vision Tanzania
Muonekano wa sehemu ya vifaa tiba na vifaa kinga vilivyotolewa na World Vision Tanzania
Picha ya kumbukumbu baada ya makabidhiano ya vifaa tiba na vifaa kinga vilivyotolewa na World Vision Tanzania
Mhasibu Mkuu wa World Vision Kanda ya Ziwa Bw. Lukelo Kivambe na Kaimu Meneja wa Shirika la World Vision Kanda ya Ziwa Bi. Irene Abusheikh (katikati) wakiagana na Kaimu Mganga Mkuu Mkoa wa Shinyanga Rad. Faustine Mulyutu baada ya makabidhiano ya vifaa tiba na kinga kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa wa Kipindupindu.
 
Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog 

About the author

mzalendoeditor