Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume – Zanzibar. Leo tarehe 11 Januari 2024 Makamu wa Rais anatarajia kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Skuli ya Elimu Mjumuisho ya Jendele iliyopo Wilaya ya Kati, Unguja ikiwa ni shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. Tarehe 11 Januari 2024.