Uncategorized

WAZIRI MKENDA ARIDHISHWA NA MIUNDOMBINU YA KISASA SHULE YA SEKONDARI YA MFANO DODOMA

Written by mzalendo

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda,akimsikiliza Mkurugenzi wa Kampuni ya Biogas and Solar Mhandisi Ainea   Kimaro wakati akikagua ukamilishaji shule ya sekondari ya Mfano iliyopo Iyumbu Dodoma iliyojengwa na Wizara hiyo leo Januari 9,2024 jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna-DODOMA

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda amepiga marufuku shule kuweka michango ya lazima ambayo inawanyima watoto kwenda shule.

Waziri Mkenda ametoa kauli hiyo leo Januari 9,2024 jijini Dodoma wakati akikagua ukamilishaji shule ya sekondari ya Mfano iliyopo Iyumbu Dodoma iliyojengwa na Wizara hiyo pamoja na Ujenzi wa Jengo la Wizara hiyo lililopo Mji wa Serikali Mtumba.

“Ni marufuku kwa shule yeyote kuweka michango ya lazima ambapo mzazi au mtoto asipotoa mchango huo mtoto atakatazwa kwenda shuleni. Rais wetu Samia Suluhu Hassan amekamilisha utaratibu wa kutoa elimu bila ada mpaka kidato cha sita hatutarajii mzazi aambiwe atoe mchango wa lazima,”amesema Prof.Mkenda

Hata hivyo Prof.Mkenda amewapongeza  wazazi wanatoa michango yao kwa hiari na kusisitiza mtoto asirudishwe nyumbani kwa kutochangia dawati au chochote.

Aidha Waziri Mkenda ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Dodoma City inayojengwa na Wizara hiyo maarufu kama Shule ya Mfano.

Prof.Mkenda amesema kuwa kwa hatua iliyofikia ni kuwa Wizara iko tayari kwa uzinduzi kabla ya kuikabidhi Ofisi ya Rais TAMISEMI.

“Tunatarajia kufanya uzinduzi na tutakabidhi TAMISEMI na tumefurahishwa na ubunifu uliofanywa na SUMA JKT kwa kutengeneza gesi yao wenyewe kwa kutumia maji machafu ili kupunguza gharama za uendeshaji wa shule,”amesema Prof.Mkenda

Hata hivyo, amesema kuwa mwaka ujao wa masomo wa kidato cha tano na sita itachukua wanafunzi wa tahsusi za sayansi kwa kuwa lengo la serikali ni kuzalisha wataalamu wengi wa sayansi watakaosaidia kada mbalimbali.

Aidha Waziri Mkenda amempongeza Mkandarasi wa mragi huo kwa kufanya kazi nzuri kwa ubunifu wa kutengeneza mfumo wa maji taka utaoka wezesha kuzalisha gesi kwa kutoa maji kwa ajili ya umwangiliaji.

Kwa upande wake Meya wa Jiji la Dodoma Prof. Devis Mwamfupe amesema kuwa Shule hiyo ni jitihada za dhati za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kutaka Watoto wa kitanzania kupata elimu bora na katika Mazingira bora na kumshukuru Kwa kuchagua Dodoma kujengwa Shule hiyo ya Mfano.
“Serikali ya Awamu ya Sita Chini Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuhakikisha Elimu inatolewa Kwa viwango vikubwa ndio maana Shule za siku hizi zinajengwa Kisasa na Shule hii ya Mfano hapa Iyumbu ni Moja ya Shule Bora,”amesema Prof. Mwamfupe

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Suma JKT, Kanali Petro Ngata,amesema Mradi huo wa Ujenzi wa Shule hiyo imefikia Asilimia 96 kukamilika.

”Tunaishukuru  serikali kwa kuiamini Suma JKT kutekeleza miradi mikubwa nchini na ujenzi wa mradi huo ulianza Mwaka 2020 na hadi mwishoni mwa Januari mwaka huu utakuwa umekamilika.”amesema Kanali Ngata

   

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda  akikagua ukamilishaji shule ya sekondari ya Mfano iliyopo Iyumbu Dodoma iliyojengwa na Wizara hiyo leo Januari 9,2024 jijini Dodoma.

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda,akimsikiliza Mkurugenzi wa Kampuni ya Biogas and Solar Mhandisi Ainea   Kimaro wakati akikagua ukamilishaji shule ya sekondari ya Mfano iliyopo Iyumbu Dodoma iliyojengwa na Wizara hiyo leo Januari 9,2024 jijini Dodoma.

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda,akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 9,2024 mara baada ya kukagua   ukamilishaji shule ya sekondari ya Mfano iliyopo Iyumbu jijini Dodoma iliyojengwa na Wizara hiyo .

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda,akiwa katika picha ya pamoja  mara baada ya kukagua  ukamilishaji shule ya sekondari ya Mfano iliyopo Iyumbu jijini Dodoma iliyojengwa na Wizara hiyo .

Muonekano wa ujenzi wa jengo la Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia linalojengwa katika Mji wa Serikali Mtumba Dodoma.

About the author

mzalendo