Leo tarehe 6 Januari 2024, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewasili Zanzibar, Mkoa wa Kusini Pemba kwa ajili ya ziara ya kikazi.
Katika Uwanja wa Ndege wa Pemba, Dkt. Biteko amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mhe. Mattar Zahoro, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Jumanne Sagini na viongozi wengine wa Serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM).