Uncategorized

DKT. TULIA ACKSON, ASHIRIKI UFUNGUZI WA MKUTANO WA 27 WA MASPIKA NA WENYEVITI WA MABUNGE WANACHAMA WA JUMUIYA YA MADOLA

Written by mzalendo

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, ameshiriki hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa 27 wa Maspika na Wenyeviti wa Mabunge Wanachama wa Jumuiya ya Madola uliofanyika leo tarehe 4 Januari, 2024, Kampala nchini Uganda. Mkutano huo umefunguliwa na Rais wa nchi hiyo Mhe. Yoweri Kaguta Museveni.

Mkutano huu pamoja na mambo mengine unatoa fursa kwa Maspika hao kubadilishana uzoefu wa uendeshaji bora wa Mabunge yao. Katika mkutano huo unaoendelea mada mbalimbali zitawasilishwa na kujadiliwa ikiwemo masuala ya mazingira na mabadiliko ya tabia nchi, masuala ya jinsia na ushirikishwaji wa vijana pamoja na ujengaji wa misimamo ya pamoja ya kibunge

About the author

mzalendo