Uncategorized

KAMATI YA BUNGE UTAWALA, KATIBA NA SHERIA

Written by mzalendo

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imeanza Vikao vyake leo tarehe 03 Januari 2024.

Aidha Kamati hiyo pamoja na mambo mengine imepanga kupokea maoni ya Wadau kuhusu Miswada minne iliyosomwa Bungeni Mara ya Kwanza wakati wa Mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge.

Miswada hiyo ni pamoja na; Muswada wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2023; Muswada wa Sheria ya Tume ya Uchaguzi wa Mwaka 2023; Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na.5) wa Mwaka 2023 [The Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No.5) Bill, 2023]; na Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria za Vyama vya Siasa wa Mwaka 2023 [The Political Affairs Laws (Amendment) Bill, 2023].

Vikao vya kupokea maoni ya Wadau vitafanyika tarehe 6, 8 hadi 10 Januari, 2024 Ofisi ya Bunge, Jijini Dodoma.

About the author

mzalendo