Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limefanikiwa kuwakamatawatu wanne ambao ni Ramadhani Mdoe (30) mkazi wa Msamvu akiwa na wenzake Watatu wakiwa wanatengeneza na kusambaza bidhaa feki ya pombe kali wanayoifananisha na Smart Gin pamoja na Konyagi katika kiwanda kisicho sajiliwa (Kiwanda bubu) kilichopo mtaa wa Tushikamane Kata ya Lukobe Manispaa ya Morogoro Disemba 28, 2023.

Watuhuniwa hao wamekutwa na chupa zilizojazwa pombe feki inayofanana na Smart Gin 2544, chupa tupu 2988, Chupa zilizojazwa pombe feki inayofananishwa na Konyagi 65, chupa tupu mbalimbali za konyagi zikiwa ndani ya mifuko minne ya salfeti, box moja, madumu ya lita 20 yaliyojazwa spiriti 4, Pipa tupu moja la spiriti, Dumu 6 za lita 20 zenye mchanganyiko wa spiriti na maji, Dumu moja la lita 13 lenye mchananyiko wa spiriti na maji, Dumu 4 tupu za lita 20, Dumu 6 tupu za lita 13, Dumu 6 za lita 13 zenye maji, mifuko 6 ya salfeti na maboksi 2 makubwa yenye maboksi ya Konyagi, Jaba 3 kwa ajili ya kuchanganya na kuchuja Pombe hiyo, Gundi chupa 5, PM kwaajili ya ladha, Stika feki 2037 za TRA, Lebo 6226 za Smart Gin pamoja na Lebo za konyagi kubwa na ndogo 10,886.

Watuhumiwa hawa wanashikiliwa kwenye Kituo kikubwa cha Polisi kwa ajili ya mahojiano kabla ya kufikishwa Mahakamani kwa hatua zaidi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro ACP Alex Mkama amesema, Watuhumiwa hawa wamekamatwa ikiwa ni muenedelezo wa misako na operesheni inayoendelea katika Mkoa wa Morogoro, na hii ni kutokana na ushirikiano unaotolewa na Wananchi kwa Jeshi la Polisi baada ya kuwapa elimu ya kutosha kupitia Polisi Kata.

Aidha, Kamanda Mkama amesema, Operesheni na misako hii ni endelevu na haitamuacha salama mtu yeyote anayefanya vitendo vya kihalifu na kuwataka waache au kujisalimisha wenyewe.

Vilevile amewaomba Wananchi kuendelee kufichua wahalifu kwa kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi ili zifanyiwe kazi na kufanya Mkoa kuwa salaama.

Previous articleSAGINI AFUNGA MAFUNZO YA AWALI KOZI NA. 31/2023 CHUO CHA MAGEREZA KIWIRA
Next articleSERIKALI YATOA MISAADA YA KIBINADAMU KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO KILIMANJARO

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here