Kitaifa

SAGINI AFUNGA MAFUNZO YA AWALI KOZI NA. 31/2023 CHUO CHA MAGEREZA KIWIRA

Written by mzalendo

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Jumanne Sagini (Mb) amefunga Mafunzo ya Awali Kozi Na. 31/2023 katika Chuo cha Magereza kilichopo Kiwira Wilaya ya Rungwe Jijini Mbeya Desemba 29, 2023.

Katika Hotuba yake Mhe. Sagini alieleza kuwa, Kwa upande wa Jeshi la Magereza, Mhe. Rais na Amiri Jeshi Mkuu katika kipindi cha Uongozi wake kwa mwaka wa fedha 2022/2023 na 2023/2024 Jeshi la Magereza lilipewa pesa kiasi cha Tsh. Bilioni 7,280,000,000/= ambazo zilitumika kujenga makazi 191 ya Askari, Wakaguzi na Maafisa nchi nzima.

“Serikali ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendeleea kutoa pesa ya mafunzo mbalimbali kwa Vyombo vya Usalama ili kuimarisha uwezo wa ulinzi wa vyombo vyetu, katika Jeshi letu la Magereza Mhe. Rais alitoa pesa zilizowesha kupandisha vyeo kwa mfululizo kwa Askari, Wakaguzi na Maafisa wapatao 14,479 zikiwemo na ajira mpya”. Alisema Mhe. Sagini

Pia Mhe. Sagini alimshukuru Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia uboreshaji wa Shirika la Uchumi la Magereza (SHIMA) kufanyiwa mabadiliko yaliyoleta ufanisi na tija katika shirika ikiwa ni pamoja na ongezeko la uzalishaji wa mazao ya kilimo, mifugo, viwanda vidogo vidogo na ujenzi.

Aidha, alitoa rai kwa wahitimu kutumia mafunzo waliyoyapata yawasaidie kufanya kazi kwa weledi, umahiri na usasa zaidi kwenye kuwasimamia na kuwarekebisha wafungwa na mahabusu kwa kuzingatia Sheria, kanuni na miongozo itolewayo mara kwa mara na viongozi.

“Niwapongeze kwa suala zima la usafi kwa kuzingatia misingi ya afya kwa kufuata miongozo na maagizo mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa na wataalamu wa afya katika kulinda afya zenu ikiwemo namna bora ya kujikinga na ugonjwa wa UKIMWI na magonjwa mengine ya kuambukiza na niwasisitize kuendelea na tahadhari mlizopewa hata mtakapoenda kwenye vituo vyenu vya kazi Wizara na Serikali inahitaji kuwa na Watumishi wenye afya bora wakati wote ili kutekeleza majukumu yao vizuri”. Alisema Mhe. Sagini

Kwa upande wake Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza CGP Mzee Ramadhani Nyamka alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

About the author

mzalendo