Jeshi la Polisi Mkoani Manyara limebainisha kuwa matumizi ya dawa za kulevya na ulevi kupindukia kwa baadhi ya watu katika jamii ndio vinavyowasababishia kujiingiza kwenye kutenda matukio ya kihalifu kinyume Cha sheria
Hayo amesema Kamanda wa Polisi Mkoani humo Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) George Katabazi mapema Desemba 26, 2023 wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake waliotaka kujuwa Jeshi Hilo limebaini nini chanzo Cha uhalifu Mkoani humo
Pia ameeleza matumizi ya dawa za kulevya na pombe hupelekea katika kufanyika kwa uhalifu mwingine kama unyang’anyi, wizi na hata kubaka hivyo amesisitiza vita ya kupinga matumizi ya dawa za kulevya na Pombe kupita kiasi ni mtambuka yanayohitaji ushirikiano baina ya Jeshi hilo na Jamii
“Jamii tushirikiane kukemea matumizi ya dawa za kulevya kwani vijana wengi wakishatumia hujiingiza katika kufanya uhalifu hususani ukatili wa Kijinsia” alisema Katabazi
Aidha, ameeleza Doria na Operesheni za kuwakamata watuhumiwa wa dawa za kulevya hususani Bangi na mirungi pamoja na Pombe haramu ya Moshi maarufa kama Gongo bado zinaendelea maeneo mbalinbali ya Mkoa huo na amewaomba wananchi kushirikiana na Polisi katika Kubaini, kutanzua na kuzuia uhalifu na wahalifu
Jeshi la Polisi Mkoani hapa limewataka wananchi wanaojihusisha na biashara ya Dawa za Kulevya pamoja na pombe haramu ya Moshi kuacha mara moja kwani halitakuwa na muhali kwa mtu au kikundi kitakachojihusisha
Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Manyara amesema kwa kushirikiana na vikundi vya Ulinzi pamoja na Jamii kwa ujumla watazidisha vita na kutokomeza matumizi ya dawa za kulevya pamoja na pombe haramu ya Moshi katika kukabiliana na uhalifu na wahalifu Mkoani humo