Mahakama ya Wilaya ya Babati imeifutilia mbali kesi ya ukatili iliiyokuwa ikimkabili mbunge wa Babati Mjini, Pauline Gekul kuhusiana na tuhuma za unyanyasaji dhidi ya mfanyakazi wake, Hasim Ally.
Kwa mujibu wa Mwananchi, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Babati, Victor Kimario ameieleza kuwa kesi hiyo imetajwa leo Jumatano Desemba 27, 2023 mbele yake na ameifuta baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kuwasilisha taarifa va kutokuwa na nia va kuendelea navo.
“DPP amewasilisha taarifa ya kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi)”, amesema Hakimu Kimario na kufafanua kuwa, hakuna wakili wa Serikali alivefika mahakamani leo wakati kesi hivo ilipotajwa na taarifa hivo wamewasilisha masjala.
Kesi hiyo ilifunguliwa na Hashimu kupitia kwa wakili Peter
Madeleka chini ya kifungu cha 128(2) na (4) cha Sheria ya
Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2022.
Wakili Madeleka alilieleza Mwananchi kuwa kifungi hicho kinaruhusu mtu binafsi kufungua kesi ya jinai bila kupitia kwa DPP.
Kwa mujibu wa hati hiyo ya malalamiko ya kesi hiyo, Gekul alikuwa anakabiliva na shtaka moja la shambulio na kusababisha madhara kwa mwili chini ya kifungu cha 241 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16, marekebisho ya mwaka 2022.
Alikuwa anadaiwa kuwa yeye na watu wengine ambao hawako katika malalamiko hayo, Novemba 11, 2023, mjini Babati, mkoani Manyara walimuita Hashim na kumuweka kizuizini, huku wakimtishia kwa silaha ya moto, walimvua nguo na kumshambulia kwa kumlazimisha kukalia chupa ya soda ili iingie katika njia yake ya haja kubwa.
DPP amewasilisha taarifa hivo ya kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi hiyo chini ya kifungu cha 91(1) cha CPA, kinachompa mamlaka ya kufuta kesi yoyote ya jinai katika hatua voyote kabla ya hukumu va Mahakama na bila kulazimika kutoa sababu za uamuzi huo.
Chanzo cha habari Mwananchi.