Featured Michezo

WALIO KULA 5 KWA YANGA WATOSHANA NGUVU

Written by mzalendo
TIMU ya Simba SC imelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na KMC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara mchezo uliopigwa  Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
Mabao ya KMC yamefungwa na mshambuliaji  Waziri Junior Shentembo akimtungua kipa, wa Simba  Ayou Lekred dakika ya 31 na la pili la kusawazisha dakika ya 88.
Kwa upande wao Simba SC mabao yao yamefungwa na kiungo Mshambuliaji, Saido Ntibanzokiza dakika ya 57 kwa penalti na mshambuliaji Jean Baleke dakika ya 81.
Simba SC inafikisha pointi 23,ikiwa  nafasi ya tatu ikizidiwa pointi nne na mabingwa watetezi, Yanga baada ya wote kucheza mechi 10 na wote wapo nyuma ya Azam FC inayoongoza kwa pointi zake 31 za mechi 13.
KMC kwa upande wao baada ya sare ya  wanafikisha pointi 21 na kusogea nafasi ya nne wakiizidi Singida Fountain Gate pointi moja ambayo sasa inahamia nafasi ya tano baada ya wote kucheza mechi 14.

About the author

mzalendo