Featured Kitaifa

RAIS SAMIA AANZISHA MPANGO WA MADAKTARI BINGWA KUWAJENGEA UWEZO WATUMISHI VITUO VYA AFYA

Written by mzalendoeditor

Na. WAF – Tanga

Rais wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ameanzisha mpango wa Madaktari Bingwa kwenda kuwajengea uwezo watumishi katika vituo vya Afya ili waongeze utendaji wao katika kuwahudumia wananchi kwa ufanisi.

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema hayo Jana Disemba 22, 2023 wakati akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Tanga.

“Mpango huu ni mahususi kwa ajili ya kupunguza vifo vya mama na mtoto na kuimarisha utoaji wa huduma bora katika vituo vya Afya kote nchini.” Amesema Waziri Ummy

Aidha, Waziri Ummy amesema kuwa ili kufanikisha mpango huo, kiashi cha Tsh: Bilioni 625 kutoka benki ya Dunia zitatumika katika kuhakikisha mpango huo unakuwa endelevu na kuvifikia vituo ambavyo havijafikiwa nchi nzima.

“Hii ni awamu ya pili ya madakitari bingwa wa Mama Samia wanaozunguka katika vituo vya Afya kote nchini kwa kutoa huduma na kuwajengea uwezo watumishi ili kuwajengea uwezo katika utendaji kazi wao.” Amesema Waziri Ummy

About the author

mzalendoeditor