Featured Kitaifa

MAKAMU WA RAIS AKABIDHI ZAWADI KWA WATOTO YATIMA

Written by mzalendo

Msaidizi wa Sheria wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bw. Elisha Suku (mwenye koti jeusi) akikabidhi zawadi kutoka kwa Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Mpango katika Kituo cha Kulea Watoto Yatima cha Jerusalem Home of God’s Love For Children kilichopo Kimara Jijini Dar es salaam. Watatu kutoka kushoto ni Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani Usharika wa Kimara Jijini Dar es salaam Wilbroad Matsai.

Msaidizi wa Sheria wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bw. Elisha Suku (mwenye koti jeusi) akiwa katika picha ya pamoja na watoto wanaolelewa katika Kituo cha Kulea Watoto Yatima cha Jerusalem Home of God’s Love For Children kilichopo Kimara Jijini Dar es salaam mara baada ya kukabidhi zawadi kutoka kwa Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Mpango. Wengine katika picha ni walezi wa kituo hicho pamoja na  Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani Usharika wa Kimara Jijini Dar es salaam Wilbroad Matsai.

………..

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amekabidhi zawadi katika Kituo cha Kulea Watoto Yatima cha Jerusalem Home of God’s Love For Children kilichopo Kimara Jijini Dar es salaam. Zawadi hizo ni pamoja na vyakula, vinywaji, sabuni, mafuta ya kupikia pamoja na mavazi. 

Akikabidhi zawadi hizo Msaidizi wa Sheria wa Makamu wa Rais Bw. Elisha Suku amesema Makamu wa Rais ametoa zawadi hizo kwa lengo la kusheherekea pamoja na watoto hao sikukuu za Krismasi na Mwaka mpya. Aidha ameongeza kwamba Makamu wa Rais amewatakia heri na afya njema watoto pamoja na walezi wao.

Akizungumza mara baada ya kupokea zawadi hizo, Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani Usharika wa Kimara Jijini Dar es salaam Wilbroad Matsai amemshukuru Makamu wa Rais kwa zawadi hizo pamoja na viongozi wote wanaojitoa kwaajili kwaajili ya kusaidia wenye uhitaji.

About the author

mzalendo