Featured Michezo

UWANJA WA CCM MAJIMAJI KUFANYIWA UKARABATI .

Written by mzalendo

Na, Brown Jonas – WUSM,

Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekabidhi mashine mbili za kukatia nyasi katika uwanja wa mpira wa miguu wa CCM Majimaji kwa uongozi wa chama hicho Mkoa wa Ruvuma.

Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekabidhi mashine hizo leo Desemba 21, 2023 mjini Songea ikiwa ni utekelezaji wa azma ya Serikali kufanya maboresho katika viwanja mbalimbali nchini.

Amesema kuwa kukarabatiwa kwa uwanja huo kutawezesha vilabu  mbalimbali nchini kuutumia uwanja huo kwa mechi za ligi kuu jambo ambalo litaongeza hamasa ya soka mkoani humo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Ndg. Odo Mwisho ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa jitihada mbalimbali inazofanya kuboresha sekta ya michezo nchini hususani mkoa wa Ruvuma ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya  mwaka 2020-2025.

Makabidhiano ya mashine hizo zenye thamani ya Shilingi Milioni  saba  yameshuhudiwa na Mkuu wa Wilaya ya Songea Mjini Bw. William Kapenjama na viongozi wengine wa chama na serikali ambapo pia Mbunge wa Jimbo hilo na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amemleta mtaalam atakayetoa mafunzo kwa  wasimamizi wa uwanja kuhusu matumizi ya mashine hizo uwanjani hapo.

About the author

mzalendo